Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya
visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la
Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200
kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati
mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe
pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la
msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine
katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika AfDB Alex Mubiru.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa
wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika sherehe
zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa Arumeru
jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wananchi wa Arumeru mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji
safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha.
Wananchi
wa Arumeru wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Arumeru.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka katika
eneo la mkutano.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro
mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment