Diwani wa Kata ya Dunda Dickson Makamba akizungumza katika hfla hiyo.
..................................
..................................
Na Omary Mngindo,
Bagamoyo
JUMUIA ya Wazazi wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani inatarajiwa kuandaa harambee kubwa katika Kata ya
Dunda inayolenga kupatikana kwa fedha zilizotumika kumalizia Bweni sekondari ya
Kata.
Mjumbe Kamati ya
Utekelezaji jumuia hiyo Wilaya Yahya Msonde, aliyemwakilisha Mwenyekiti wa
Jumuia hiyo wilaya Aboubakary Mlawa, katika hafla ya kupongezwa walimu katani
humo kwa kufanikisha Kata hiyo kuwa ya kwanza kiwilaya.
"Nilipopewa taarifa
na Mwenyekiti wangu Mlawa kuja kumwakilisha kwenye hafla hii, nilijiuliza
mara milimbiko nini cha kuzungumza, lakini kwa kuwa nami ni mdau wa elimu
siwezi kukosa la kuzungumza, lakini la kwanza niwasilishe hili la
Harambee inayohimizwa ifanyike wiki ya kwanza mwezi Januari, " alisema
Msonde.
Akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi, diwani wa Kata ya Dunda Dickson Makamba alianza kwa
kuwapongeza walimu kwa kazi kubwa wanavyoendelea kuifanya katani humo,
akisemaa kwamba huu ni mwaka wa tatu mfululizo kushika nafasi hiyo.
"Niwashukuru walimu
kwa kujitoa kikamilifu katika kuhakikisha Kata ya Dunda inaendelea kuwa kinara
katika imu, pia wazazi, walezi na wadai mbalimbali wanaoendelea kusaidia katika
nyanja tofauti za kuhakikisha elimu inaendelea kuboreshwa katani hapa,"
alisema Makamba.
Akizungumzia changamoto ya
Bweni kwenye shule ya Kata, Makamba alisema kuwa kuna juhudi nyingi
zinazoendelea kufanyika akiwemo Mwenyekiti wa Jumuia hiyo aliyechangia mabati
100, lengo kuhakikisha wanafunzi wanakaa shuleni.
"Mbali ya Jumuia pia
kuna wadai wengi ambao wamechagia ujenzi wa Bweni akiwemo Mbunge wa Jimbo
Dkt. Shukuru Kuwambwa aliyechanga mifuko 100 ya saruji pamoja na wadau
wengi waliojitolea na wengine bado wanaendelea kujitokeza kusaidia elimu katani
Dunda, " alisema Makamba.
Mwalimu Mkuu shule ya
Mwambao Alpu Mwegeho akitoa shukrani kwa niaba ya walimu wenzake, alitoa kilio
cha kucheleweshwa mafao ya walimu hali inayopunguza hamasa ya walimu wilayani
humo.
Mwakilishi wa wazazi Ummy
Matata amepongeza juhudi za walimu, huku akisema kwamba kwa miaka mingi suala
la ufaulu katani humo halikuwepo, huku akimpongeza Diwani Makamba kwa
kushirikisha watu mbalimbali.
Taarifa ya Walimu katani
humo iliyosomwa na Saad Momba mwalimu shule ya Msingi Mwambao inazungumzia
changamoto ya ukosefu wa kompyuta hali inayochangia kupunguza uwezo wa
wanafunzi katika elimu.
Mjumbe Kamati ya Utekelezaji jumuia ya wazazi Wilaya, Yahya Msonde, ambae alikuwa mgeni rasmi kumuwakilisha Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
Mjumbe Kamati ya Utekelezaji jumuia ya wazazi Wilaya, Yahya Msonde,akikabidhi zawadi kwa mwalimu Amina Ally wa shule ya msingi MWASAMA.
Mjumbe Kamati ya Utekelezaji jumuia ya wazazi Wilaya, Yahya Msonde,akikabidhi fedha taslimu shilingi laki moja kwa mwalimu
Mjumbe Kamati ya Utekelezaji jumuia ya wazazi Wilaya, Yahya Msonde, akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti CCM kata ya Dunda, Mwinyi Hashim Akida.
No comments:
Post a Comment