Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jeneral Venance Mabeyo akipokea mkono wa Heri ya
Krismasi kutoka kwa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus
Sangu, katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango
cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika
Desemba 26, 2018.
Askofu
wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu akimshuhudia Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati akitia saini kama
shahidi katika Hati ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Mtakatifu
Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya, katika ibada ya kubariki na
kutabaruku kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
.................................................
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini Jenerali
Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea kuhubiri amani
ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na mshikamano.
Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa ibada ya
kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia
ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa
akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Naibu Gavana wa Benki
Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama na Serikali, ambapo
alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo kwa Taifa lolote duniani.
“Suala la amani na utulivu ni la msingi sana
katika nchi yetu, kwa vile kila mwananchi ana dini yake tunaamini kuwa viongozi
wa dini zote kwa kuwa wanasikilizwa sana na waumini wakiweka
msisitizo katika suala la amani, amani itatawala na kutakuwa na utulivu”
“Utulivu huu tunauhitaji sana ili tupate
maendeleo, kama viongozi wetu wa kisiasa wanavyosisitiza kuwa tudumishe
amani na utulivu tupate maendeleo, bila utulivu watu wakiwa wanahaingaika
hakuna maendeleo kwa sababu hakuna shughuli mtu anaweza kufanya kama hana amani
na utulivu, hivyo hataweza pia kuleta maendeleo yake, familia, jamii na Taifa
kwa ujumla” alisema Jenerali Mabeyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema vitendo vingi vya uvunjifu wa amani na
uhalifu ikiwemo ukataji wa mapanga na mauaji ya vikongwe na yanachangiwa na
watu kukosa hofu ya Mungu; hivyo nyumba za ibada(makanisa na misikiti)
zinapojengwa kwa wingi zitakuwa msaada mkubwa sana kwa watu kuwa na hofu ya
Mungu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
amesema jamii inayoamini uwepo wa Mungu haiwezi kuwa na vitendo vya kisasi,
kukatana mapanga na mauaji ya vikongwe huku akiwaasa Watanzania kukaa kwa amani
na upendo bila kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha amani.
Akibariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro,
Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega, Askofu wa Jimbo
Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu amewataka Watanzania kupendana na
kuacha roho ya ubinafsi na visasi.
Aidha, Askofu Sangu ametoa wito kwa viongozi na
waumini kufanya nyumba za ibada zibaki nyumba za sala kama yanenavyo maandiko
matakatifu na kamwe zisitumike kama majukwaa
la wanasiasa.
” Palipo na msamaha pana umoja, uelewano na usawa
lakini palipo na kisasi hapana maendeleo; nyumba ya ibada isitumike kama jukwaa la Wanasiasa alisisitiza Muhashamu Askofu
Sangu.
Kutoka
kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Naibu Gavana wa Benki
Kuu, Dkt. Benard Kibese, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,Mkuu wa
Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance
Mabeyo wakiwa katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro
Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu,
iliyofanyika Desemba 26, 2018.
No comments:
Post a Comment