MNEC wa mkoa wa pwani
(kushoto) akimsikiliza mwenyekiti wake katika kikao na watendaji wa CCM wilaya zote za
mkoa wa Pwani.
......................................................
Na Shushu
Joel, Kibaha.
MWENYEKITI
wa ccm mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno amewaagiza watendaji wa chama hicho
kuacha kufanya kazi kwa mazoe kama walivyokuwa wamezoea miaka ya nyuma.
Watendaji wa
Ccm walio wengi wameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano chini ya
mwenyekiti wa taifa Dkt John Pombe Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania kwa
watendaji wengi kufanya kazi za chama kipindi cjha chaguzi tu.
Akizungumza
na watendaji wa mkoa huo mwenyekiti huyo aliwataka watendaji wote kuwajibika
kwa wanachama wa chini katika kuwasaidia kutambua sitahiki zao kwani wanachama
wa chini wamekuwa wakinyanyaswa na matajili huku viongozi wa chama wakiangalia
tu na kushindwa kuwajibika katika kuwasaidia ili waweze kupata haki zao.
“Watendaji
wa chama wamekuwa wajijisahau katika uwajibika wao na kibaya zaidi wamekuwa ni
watu wa kuagiza tu huku wakiwa wamekaa ofisini”Alisema
Aliongeza
kuwa watendaji wa chama ndio mhimiri mkubwa katika chama hivyo ni lazima
watendaji wote katika mkoa wahakikishe wanakuwa ni kiungo kikubwa kati ya
uongozi na wanachama wea chini.
Aidha
amewataka watendaji kuwa wabunifu katika kipindi hiki kutokana na kuwa kipindi
cha sasa ni kipindi cha siasa ni uchumi kwa kuwaelimisha wanachama juu ya
umuhimu wa kuwa na vikundi vilivyosajiliwa katika vyombo husika ili waweze
kukopesheka na kujijengea uchumi wao ambao utawatoa katika kipindi cha kuwa
omba omba kwa watu.
Kwa upande
wake mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa kupitia mkoa wa Pwani (NEC)Haji Jumaa
amempongeza mwenyekiti huyo kwa kuona umuhimu wa kukutana na makatibu wote wa
mkoa wa Pwani na kuwakumbusha wajibu wao katika utendaji.
Aliongeza
kuwa watendaji wakisimama imara katika usimamizi wa mali za chama hali ya ccm
itakuwa zaidi ya hapo ilipo sasa.
“Makatibu
wanapaswa kuwajibika kwa bidii ili kuhakikisha chama chetu kinazidi kuwa bora
kuanzia ngazi za mashina mpaka taifa na hii inawezekana pale kila mmoja
atahakikisha anakuwa mkali kwa yule mwenye nia mbaya na chama katika kutumia
mali za chama ovyo”Alisema Jumaa.
Aliongeza
kuwa zoezi la kuwasajili wanachama wa ccm kwa njia ya kielectronic ni jema
kwani liwaongeza mapato ya chama na kukifanya chama kuwa juu zaidi ya hapo
kilipo sasa.
Naye katibu
wa ccm wilaya ya Kibaha vijijini Janeth Mnyaga ameupongeza uongozi wa ccm mkoa
kwa kuwakutanisha na kuwataka kuwajibika katika shughuli zao za usimamizi wa
chama katika ngazi za wilaya.
Hivyo
aliongeza kuwa elimu iliyotolewa leo kwa watendaji wote iwe endelevu kwani
inawapatia motisha katika uwajibikaji na usimamizi wa chama katika ngazi za
wilaya.
Makatibu
wa CCM mkoa wa Pwani wakimsikiliza mwenyekiti wa mkoa huo akitoa maelezo juu yao.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Pwani Ramadhani Maneno aliyesimama akitoa maelekezo kwa watendaji wa chama
hicho.
No comments:
Post a Comment