Baadhi ya Maafisa wa Polisi
walioshiriki Operesheni Nzagamba awamu ya pili wakifuatilia kwa
makini Hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina (hayupo pichani).
........................................
Na Frank Mvungi- MAELEZO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina
ameagiza Kuondolewa mara moja kwa watumishi wa Wanaosimamia Kituo cha Ukaguzi
Kibaha Mkoani Pwani kwa kushindwa kusimamia rasilimali za Sekta ya Mifugo na
Uvuvi. Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Tathmini ya
Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili iliyofanyika kati ya mwezi Oktoba na
Novemba 2018 ikilenga Kuinua mchango wa Sekta ya Mifugo katika Pato la Taifa
Waziri Mpina amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kudhibiti upotevu wa mapato ya
Serikali yatokanayo na biashara ya Mifugo na Mazao yake.
“ Watumishi wote walioshiriki katika Operesheni
Nzagamba Awamu ya Pili wamefanya kazi kubwa na kwa uzalendo mkubwa hivyo
nawapongeza kwa kuwa mmeonesha kuwa tunao uwezo wa kusimamia rasilimali zetu
ili zitoe mchango stahiki katika pato la Taifa”.Alisisitiza.
Mhe.
Mpina. Akifafanua amesema watumishi wasio waadilfu na wanaoshindwa
kutekeleza majukumu yao
hawana nafasi katika Wizara hiyo ndio maana ameagiza kuondolewa mara moja kwa
watumishi wanaofanya kazi ya ukaguzi wa rasilimali hizo katika kituo cha
Kibaha.
Aliongeza kuwa Operesheni Nzagamba awamu ya Pili,
2018 imedhihirisha kwamba usimamizi thabiti wa Sheria, Kanuni na Taratibu
katika Sekta ya Mifugo unaweza kuleta tija kwa kuongeza uzalishaji bora wa
mazao ya mifugo ambayo ni malighafi ya Viwanda na hivyo kuchangia ipasavyo
katika kuendeleza uchumi wa Viwanda.
“ Ni mategemeo yangu kuwa wananchi mtakuwa
wazalendo kwa nchi yetu kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Kufanya
biashara ya mifugo pia kutoa taarifa pale mnapobaini utoroshaji wa mifugo
kwenda nchi jirani bila kulipiwa ushuru na tozo stahiki ili hatua za kisheria
zichukuliwe dhidi ya watu hao”. Alibainisha Mhe. Mpina.
Pia aliwaasa
Watumishi wa Wizara hiyo na wale wa Halmashauri kuhakikisha kuwa wanasimamia
kwa makini utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zote zinazosimamia
biashara ya Mifugo na Mazao yake hususan mabadiliko ya Kanuni mpya iliyotolewa
mwezi Agosti, 2018.
Katika kuhakikisha minada yote ya awali na ile ya
Upili pamaoja na ile ya mipakani inatoa matokea chanya, Waziri Mpina amesema
kuwa usimamizi utaendelea kuimarishwa ili kuwezesha biashara ya mifugo
kufanyika kwa ufanisi na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli, tozo na
ushuru wa Serikali.
Alizitaka Mamlaka zinazotoa Leseni kwa wafanyabishara
wanaosafirisha Mifugo nje ya nchi kuweka utaratibu rafiki utakaosaidia
kundi hilo
kutoa mchango wake katika ujenzi wa Taifa na kuondoa au kupunguza vitendo vya
biashara ya magendo.
Aidha Waziri Mpina aliagiza kufunguliwa kwa Ofisi za
Kanda ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali za mazao ya mifugo hapa nchini.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.
Elisante Ole Gabriel amesema kuwa Operesheni hiyo ilishirikisha watendaji 152
waliogawanyika katika timu 14 zilizofanya kazi katika nchi
nzima.
Akizungumzia mafanikio ya Operesheni hiyo amesema kuwa kwa mfano
katika Mji wa Bunda zilikuwa zikikusanywa shilingi milioni mbili na nusu
(2.5) hapo awali ambapo kwa sasa baada ya kuimarisha ukusanyaji mapato katika
eneo hilo yamefikia milioni nane (8)kwa siku.
Udhibiti wa Biashara ya Mifugo na Mazao yake
uliofanyika kupitia Operesheni Nzagamba II kuanzia tarehe 11 Oktoba, 2018 hadi
tarehe 30 Novemba, 2018 (siku 50) umeiwezesha Wizara yangu kupitia Sekta ya
Mifugo kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 5,773,074,768. Makusanyo haya
yanapelekea Wizara hiyo katika sekta ya Mifugo tu kukusanya kiasi cha shilingi
bilioni 9,764,241,926.28 kwa kipindi cha Julai hadi Novemba, 2018 sawa na
asilimia 52.87 ya lengo lililowekwa na Wizara ya Fedha.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina
akifuatilia uwasilishwaji wa Taarifa ya Tathmini ya Matokeo ya Operesheni
Nzagamba awamu ya pili leo Jijini Dodoma.Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel,Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah
Ulega na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo.
Viongozi mbalimbali wa “Comand Post” zilizotumika
kuongoza Operesheni Nzagamba awamu ya pili (Mstari wa mbele) wakifuatilia
uwasilishwaji wa Taarifa ya Tathmini ya Matokeo ya Operesheni kutoka kwa
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Dk Felix Nandonde kutoka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi(hayupo Pichani) katika Ukumbi wa St.Gasper Jijini Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina
akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel wakati wa uwasilishwaji wa
Taarifa ya Tathmini ya Matokeo ya Operesheni Nzagamba awamu ya pili leo
Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof
Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Tathmini
ya Matokeo ya Operesheni Nzagamba awamu ya pili katika ukumbi wa
St.Gasper Leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Dk Felix
Nandonde kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akiwasilisha Taarifa ya Tathmini ya
Matokeo ya Operesheni Nzagamba awamu ya pili leo Jijini Dodoma.
Viongozi 14 wa timu zilizokuwa
zinaongoza utekelezaji wa Operesheni Nzagamba awamu ya pili wakieleza
makusanyo waliyofikia mara baada ya Operesheni hiyo kuisha, leo katika ukumbi
wa St.Gasper leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina
akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Tathmini ya Matokeo ya
Operesheni Nzagamba awamu ya pili leo Jijini Dodoma.
Picha na MAELEZO.
No comments:
Post a Comment