Sunday, December 16, 2018

BARAZA LA WAFANYAKAZI OR- TAMISEMI LAKUTANA DODOMA.

 Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la Wafanya Kazi Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) wakimsikilioza mwenye kiti wa kikao (hayupo pichani) leo katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akiendesha kikao cha Baraza la Wafanyakazi OR-TAMISEMI leo katika ukumbi wa mikutano Reform jijini Dodoma.
...........................................


Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula amewataka Wakuu wa Idara kushirikiana kwa karibu na watu wanaowaongoza ili kuleta chachu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa leo katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi OR-TAMISEMI kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Reform Jijini Dodoma.

Dk.Chaula amesema ili kupata matokeo bora katika utendaji kazi wowote lazima kuwa na ushirikiano wa karibu na watu unaowaongoza katika kufanya hivyo ndipo unaweza kupata matokeo bora katika utendaji kazi wako.

“Hivyo basi kila Mkuu wa Idara atambue kuwa yeye ni mlezi wa watu anaowaongoza na kuhakikisha kunakuwa na mawasiliano mazuri baina yao ili kutimiza dhamana tulopea ya kuwatumikia watanzania” Alisema Dk.Chaula.

Pia ameongeza kuwa kiongozi mzuri ni yule anayeshirikiana na anaowaongoza na kuweka wazi nini kinafanyika katika idara ili kuleta utendaji bora katika kutekeleza majukum  ya kila siku na kwamba kila mtu afanye kazi kwa moyo mmoja, Alisema Dk.Chaula.

Aidha baada ya kikao hicho Dk.Chaula na wajumbe wa kikao hicho kwa pamoja walifika ulipo Mji wa Kiserkali ambapo ndo Ofisi Mpya za OR –TAMISEMI zinatarajiwa kujengwa.

Dk. Chaula alimalizia kwa kusema kuwa,  katika ujenzi huo OR-TAMISEMI inatumia mfumo wa “Force Account” ambapo kila mfanyakazi wa OR-TAMISEMI anakuwa msimamizi katika ujenzi  na  kunakuwa na kamati mbali mbali ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na afya OR-TAMISEMI (TUGHE), Andrew Mramba amesema chama hicho kimeandaa tuzo maalum ya kumpongeza Katibu Mkuu Mhandisi Mussa Iyombe kwa utendaji kazi bora uliyotukuka.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), wakiwa kitika eneo linapojengwa jengo jipya la ofisi za OR –TAMISEMI leo jijini Dodoma baada ya Kikao cha Baraza la Wafanyakazi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), wakiwa kitika eneo linapojengwa jengo jipya la ofisi za OR –TAMISEMI leo jijini Dodoma baada ya Kikao cha Baraza la Wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment