Mshauri
wa Benki Kuu ya Tanzania BoT
tawi la Dodoma akifafanua jambo katika semina
hiyo inayoendelea jijini Dodoma.
..................................
WATANZANIA wameshauriwa kushiriki kikamilifu
katika minada ya dhamana za Serikali kwani faida zake ni kubwa kwa Taifa
ikiwamo kufanya shughuli za maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Mkurugenzi wa
Masoko na Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Alexander Ng’winamila wakati
akiwasilisha mada katika mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha
yalioandaliwa na BoT kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za fedha
na uchumi.
Akizungumza wakati akitoa mada inayohusu uwekezaji
katika dhamana za Serikali; faida zake kwa Taifa na wawekezaji ambapo pamoja na
mambo mengine amezungumzia umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye
midana ya dhamana za Serikali.
Amesema ametoa ombi kuendelea kuhamasisha kutolewa
kwa elimu kwa umma ili waweze kushiriki kikamilifu na hatimaye kuifanya
serikali iweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa fedha za
ndani.”Ombi letu kwa vyombo vya habari tunaomba muendelee kuelimisha umma
kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye dhamana za Serikali.
Kuna faida nyingi na mojawapo ushiriki wao
utawezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani
badala ya kwenda kukopa nje ya nchi,”alisema.
Akifafanua zaidi zinazopatikana kwenye dhamana za
Serikali ni kusaidia Serikali kugharamia bajeti iwapo kutakuwa na upungufu wa
kibajeti, kupata fedha za kuendeshea miradi ya maendeleo , kusimamia ujazi wa
fedha katika uchumi, husaidia kudhibiti mfumuko wa bei , huchagia uwepo wa soko
la upili na husaidia kuhamasisha utafutaji wa mitaji kwa taasisi zingine.
Pia amesema hutoa fursa za uwekezaji ,hivyo kuwepo
kwa ushindani katika uwekezaji mbalimbali na kusaidia kupatikana kwa riba
zinazoaminia na soko huku akieleza kwa mwananchi wa kawaida faida
za kushiriki ni nyingi kwani ni sehemu salama
kutokana na ukweli kwamba Serikali haitarajiwi kukiuka mategeo ya wadai wake
wakati wa malipo.
Ametaja faida nyingine dhamana za Serikali
zinahamishika hivyo mwekezaji anaweza kuuza muda wowote.Pia dhamana za Serikali
zinaweza kutolewa kama dhamana kwa ajili ya
mikipo na faida nyingine ni kwamba dhamana za Serikali zina kiwango cha faida
inayoridhisha.”Tunaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye
dhamana za Serikali kwa maendeleo ya Taifa letu.”
Kuhusu midana ya dhamana za Serikali amesema ipo
ya aina mbili ambapo kuna mnada wa muda mfupi ambao ni wa mwaka mmoja na mnada
wa dhamana za Serikali wa muda mrefu ambao unaanzia miaka miwili mpaka miaka
20.
Pia amesema ili mwekezaji aweze kushiriki katika
minada ya dhamana za Serikali ni lazima awe na akaunti ya uwekezaji katika
dhamana za Serikali na kwamba ufunguzi wa akaunti ya dhamana za Serikali
hufanyika kupitia kwa mawakala walioidhinishwa ambao huwasilisha.
“Wakati wa kufungua akaunti kuna taarifa muhimu
ambazo zinahitaji zikiambatanishwa na kitambulisho halali kinachotambulika na
mamlaka za nchi pamoja na namba ya mlipa kodi(TIN) ”amefafanua.
Ng’winamila
amesema fomu za kujiunga zinapatikana kupitia mawakala waliopo nchini pamoja na
kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua unapozungumzia dhamana za Serikali kwa
lugha rahisi ni kwamba Serikali inakopa kwa wananchi wake.
Mkurugenzi
wa Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tazania Bw. Alexander Nw’winamila akitoa mada
ya uuzaji wa Hati Funagani na Amana za Serikali katika semina ya waandishi wa
habari za Fedha na Uchumi inayofanyika jijini Dodoma
katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania
BoT Dodoma
ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.
Bi.
Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BoT) akitoa mchango
wake katika semina hiyo kuhusu mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mada zinazotolewa na wataalam wa Benki Kuu
ya Tanzania.
Vick
Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki akifuatilia mjadala
katika semina hiyo.
Mwanablog
kutoka Fullshangweblog Bwana John Bukuku akiwa katika semina hiyo.
Meneja
Kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT
akitoa mada kuhus hatua za kuimarisha usimamizi wa Taasisi za fedha.Bw. Nassor
Omary.
Baadhi
ya wanahabari wakijadiliana jambo katika semina hiyo.
No comments:
Post a Comment