Wakuu wa mikoa nchini
wameipongeza serikali kwa ujenzi wa Reli
ya kisasa (standard
Gauge) na kusema kuwa, huo ni mradi utakaoleta manufaa katika mapinduzi ya
kiuchumi hasa wakati huu serikali inavyojikita katika uchumi wa viwanda.
Wakiongea na Mwandishi wa
habari hizi mara baada ya kukagua Mradi huo ambapo wameanzia Morogoro hadi Dar
es Salaam wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Reli Tanzania (TRC) Bwana
Masanja Kadogosa.
Wamesema fursa nyingi
zitapatikana mara baada ya kukamilika kwa Mradi huo mkubwa hapa Tanzania na
nchi jirani.
Akizungumzia Mradi huo,
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Reli Tanzania
(TRC) Masanja Kadogosa amesema kwa sasa ujenzi huo unaenda kwa kasi ambapo
baadhi ya maeneo tayari wameanza kuweka miundombinu ikiwemo ya mataruma na
nguzo za umeme.
Kadogosa alitoa wito kwa wananchi
walio jirani na Mradi huo kutoa ushirikiano wa kutosha katika kulinda
miundombinu hiyo ambayo ni chachu ya kuleta maendeleo ikiwemo upatikanaji wa
ajira.
Wakuu wa mikoa wakipata
maelezo kuhusu ujenzi wa Reli ya kisasa
No comments:
Post a Comment