NA MWAMVUA MWINYI,
KIBITI
NAIBU waziri wa Ujenzi,
Elias Kuandikwa amesema ujenzi wa gati, uliokuwa ukisubiriwa kwa kipindi kirefu
na wakazi wa Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani umeanza ambapo shehena ya
vifaa vya ujenzi vimeanza kuwasili tayari kwa ajili ya kazi.
Aidha amewatoa wasiwasi
wakazi wa Mafia kuhusu gati la Kilindoni ,kwamba linatarajiwa kuboreshwa kwa
kuondoa dosari ndogondogo zilizopo ili liwe la kisasa.
Akizungumza na wananchi
wakati alipotembelea eneo litakapojengwa gati hilo, katika muendelezo wa ziara
yake mkoani hapo, Kuandikwa alisema ujenzi utakuwa wa miaka miwili kwa gharama
ya sh. bilioni 14 .
Alimtaka , mkandarasi wa
gati hilo kufanya kazi inayotakiwa kwa kuhakikisha, ujenzi unakamilika kwa
wakati ikiwezekana kuukamilisha kabla ya miezi 24.
Kuandikwa alisema, ujenzi
umeshaanza na mkataba ulisainiwa tarehe 24,octoba mwaka huu, ombi lake ni
kuona mkandarasi anamaliza kazi haraka.
“Fedha zipo hatutaki kuona
mkandarasi anasuasua, gati litasaidia kurahisisha usafiri kwani ndio kiu ya
wakazi wa Nyamisati na Mafia”
“Itakuwa gati la kisasa na
sasa tunakwenda kufanya maboresho katika gati la Kilindoni wilayani Mafia ili
kuwa na gati la uhakika ,kwa kuwa itazingatia ubora, teknolojia mpya kwa lengo
la magati haya yaweze kudumu kwa miaka mingi “alisisitiza Kuandikwa.
Pamoja na hayo, alielezea
ujenzi huo utakwenda pamoja na maboresho ya barabara ya Bungu -Nyamisati
itakayosaidia kurahisisha usafiri .
Akiwa barabara ya barabara
ya Mkuranga -Kisiju kiwango cha lami, yenye urefu wa 1.8km alimpongeza
meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Pwani, Yudas Msangi kwa kubana
matumizi kwenye miradi na kuweza kutumia katika miradi mingine.
Msangi alisema kwasasa
wanaendelea na kazi za kufungua na kuboresha baadhi ya barabara muhimu kuelekea
katika miradi mikubwa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment