Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya leo tarehe 08.12.2018 limeshiriki shughuli ya ujenzi na
ukarabati wa nyumba za kuishi askari katika kambi ya Field Force Unit [FFU]
Mbeya katika kuelekea maadhimisho ya miaka 57 ya uhuru wa Tanzania.
Ukarabati
huo umefanyika katika nyumba za kuishia askari ambazo zilikuwa katika hali
mbaya [chakavu] na kuzirejesha katika hali nzuri. Sambamba na hilo, Jeshi la
Polisi limeadhimia kujenga nyumba za kuishi askari katika kambi zake zilizopo
maeneo mbalimbali.
Aidha
katika kuelekea maadhimisho hayo ya miaka 57 ya uhuru, licha ya kushiriki
katika shughuli za ujenzi wa makazi ya askari, pia Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya limeshiriki katika shughuli za usafi wa mazingira katika maeneo ya
Mwanjelwa na Kabwe ikiwa ni hali ya kuhamasisha wananchi kushiriki usafi katika
makazi yao na kuunga mkono jitihada za serikali za kuhamasisha usafi wa
mazingira.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. ULRICH MATEI
ametumia fursa hii nawaomba wana Mbeya kushirikiana na Jeshi la Polisi katika
kuzuia uhalifu na kudhibiti ajali za barabarani kwa kutoa taarifa za uhalifu na
wahalifu na za madereva wasiotaka kutii sheria ili waweze kuchukuliwa hatua za
kisheria mara moja.
Aidha
amewaomba wadau wenye mapenzi mema, kuunga mkono jitihada za Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya za ujenzi na ukarabati wa nyumba za kuishi askari unaoendelea
katika kambi ya FFU
No comments:
Post a Comment