Mbunge wa viti maalum mkoani
Pwani, Subira Mgalu ameendelea kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.
Mgalu ameweza kuchangia mifuko
ya saruji 40 kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya
Mtongani na Mlandizi ambapo kata ya Mtongani Mifuko 20 na kata ya Mlandizi
mifuko 20.
Subira alitoa mifuko hiyo
ya saruji wakati alipokutana na baadhi ya viongozi wa chama ikiwa ni moja ya
kazi za kichama na kusema kuwa huo ni wajibu wakena kwamba hatochoka kushiriki
kusaidiana kutatua changamoto zilizopo kichama na serikali.
Katika Ziara aliyoifanya
Halmashauri ya Chalinze hapo jana, Subira mgalu alitoa Tenki la kuhifadhia maji
katika zahanati ya Msata pamoja na sola itakayowasaidia pindi umeme
unapokatika.
Aidha, alifika katika
Zahanati ya Pongwe Kiona na kusadia mashuka 10 kwaajili ya vitanda vya
wagonjwa.
Katika ziara yake kijiji
cha Pongwe kiona Mbunge huyo wa Viti maalum Mkoa wa Pwani, aliweka jiwe la
msingi jengo la Zahanati litakalotumika kwaajili ya kinamama kujifungulia.
Subira Mgalu ameahidi
kuchangia mifuko ya Saruji katika ujenzi huo ili kuunga mkono juhudi hizo
zilizoanzishwa na wananchi.
Diwani wa kata ya Mlandizi
Ephrasia Kadala, alisema Hili ulilolitenda ni jambo kubwa kwa wana CCM na
wananchi kijumla.
Diwani huyo aliwaomba
wadau wengine kujitolea kushirikiana ili kumaliza kero zinazowakabili kichama
katika kata hiyo.
Nae Katibu wa Jumuiya ya
wanawake (UWT) Kibaha Vijijni Janeth Mnyaga alimshukuru mbunge huyo kuwa bega
kwa bega kushiriki nao kwenye shughuli za jumuiya na chama.
Wakati huo huo Subira
alitembelea kituo cha afya Mlandizi kujionea hali ya upanuzi wa majengo kwa
gharama ya sh. Milioni 400 ambazo zimetolewa na serikali.
Madiwani wa kata ya Msata na Kimange Halmashauri ya Chalinze wamemtaja Subira mgalu kuwa ni mpambanaji asiyechoka na kwamba wanafarijika kuwa na muwakilishi mwenye kujali shida za wananchi katika eneo lake licha ya kuwa na jukumu la kitaifa katika wizara ya nishati.
Mganga mfawadhi wa Zahanati ya Msata Willy John amesema anamshukuru Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Pwani kwa msaada wa Tenki la kuhifadhia maji na pamoja sola itakayowasaidia kwa shughuli za usiku katika Zahanati hiyo
Mbunge wa viti maalum Mkoa
wa Pwani, Subira Mgalu akikabidhi Tenki la kuhifadhia maji katika Zahanati ya
Msata Halmashauri ya Chalinze.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la kina mama Zahanati ya Pongwe Kiona.
No comments:
Post a Comment