Saturday, December 1, 2018

ZIJUE STESHENI ZA RELI YA KISASA-SGR

Jumla ya Stesheni za reli ya kisasa-SGR 14 zinajengwa katika awamu mbili za Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora ambapo Stesheni kubwa ni Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma. Usanifu wa Stesheni hizi umesadifu mazingira halisi ya kitanzania, Tamaduni, madini pamoja na maliasili zinazopatikana nchini.

 Stesheni ya Dar es Salaam kwa Kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro umesadifu Madini ya Tanzanite yanayopatikana mkoani Arusha Tanzania, vituo vidogo vya Pugu, Soga, Ruvu na Ngerengere vikisadifu aina ya nyumba zinazopatikana maeneo ya Morogoro na Dodoma huku Kituo cha Morogoro kikisanifiwa kuakisi Milima ya Uruguru inayopatikana mkoani Morogoro. 

Ujenzi wa Vituo hivi vyote unazingatia mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa kuwa vitakuwa na Migahawa, Huduma za Kibenki, Maegesho ya Magari, Maduka ya Kisasa pamoja na sehemu za kupumzikia.
Stesheni ya Morogoro
Picha zikionesha Muonekano wa kituo cha Reli ya Kisasa – SGR cha Soga  kinachojengwa  Soga mkoani Pwani 
Stesheni ya Morogoro
Picha zikionesha Muonekano wa kituo cha Reli ya Kisasa – SGR cha Morogoro kinachojengwa mkoani Morogoro. Kituo hiki kitakuwa na Huduma muhimu kama Huduma za kifedha, Mgahawa, Sehemu za Kuegesha Magari na Maduka. Kituo hiki kimesanifiwa kuakisi Milima ya Uruguru inayopatikana Mkoani Morogoro

No comments:

Post a Comment