Mbunge wa Viti Maalum Mkoa
wa Pwani Zaynabu Vullu akikabidhi mifuko 20 ya Saruji kwa Mwenyekiti wa Kamati
ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa miguu wa JKT Ruvu Mlandizi Meja James kwaajili
ya ujenzi huo
.........................................
Na Omary Mngindo, Mlandizi
MBUNGE wa Viti Maalumu
Mkoa wa Pwani Zaynabu Vullu amekabidhi mifuko 20 ya saruji ikiwa ni kuunga mono
juhudi za ujenzi wa uwanja wa Moira wa JKT Ruvu uliopo Mlandizi Kibaha Pwani.
Vullu amekabidhi mifuko
hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa uwanja huo Meja James ambaye ndio
Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Ruvu, ambapo alisema mifuko hiyo ni kuunga mkono
juhudi hizo.
"Nimefarijika na
juhudi zinazoendelea za ujenzi wa uwanja wetu wa JKT Ruvu Maarufu Mabatini,
ambapo kwa ushawishi wa viongozi na wadau wameeeza kuanzisha ujenzi wa uzio wa
ukuta, nami nakabidhi mifuko 20," alisema Vullu.
Vullu aliongeza kwamba
juhudi hizo za uongozi kwa kusbirikisha wadau zinapaswa kuunga mkono katika
kufanikisha wengine kwa lengo la kufanikisha zoezi hilo muhimu.
Mbali ya Mbunge Vullu, pia
Madiwani walioambatana na mbunge huyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Fatma
Ngozi diwani wa Kaata ya Kikongo wemekabidhi mifuko mitano na kufanya mifuko
yoye kuwa 25.
Ngozi alisema kuwa uwanja
huo ambapo ni fahari kwa wana- Mlandizi, nao wameshawishika kuchangia ujenzi
huo na kwamba pia watakwenda kushaweshi wadau wengine waongezee nguvu ili
kukamilisha ujenzi huo.
Akizungumza baada ya
kupokea mifuko hiyo, Meja James alisema kwamba ujenzi huo unataraji kuchukua
tofari elfu 35 kwa gharama ya zaidi ya sh. Mil. 150 na kwamba kwa sasa
wamefikisha tofari 6,000.
"Haya matofari
mnayoyaona yamefikia 6,000 bado tunaendelea kupokea michango kutoka kwa wadau
mbalimbali wanaojitokeza kuchangia ujenzi huo, with wangu watu wengine
wajitokeze kusaidia chochote ili kukamilisha ujenzi," alisema Meja James.
Mwenyekiti wa kamati ya
ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa JKT Ruvu Mlandizi, Meja James akitoa
ufafanuzi juu ya matofali yaliyoanza kufyatuliwa tayari kwa ujenzi wa uzio huo.
Mwenyekiti wa kamati ya
ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa JKT Ruvu Mlandizi, Meja James akitolea
ufafanuzi moja ya vyumba vya kisasavilivyopo ndani ya uwanja wa JKT Ruvu Mlandizi.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulluakizungumza na kamati ya ujenzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Meja James (Picha zote na Omary Mngindo)
No comments:
Post a Comment