Na
Omary Mngindo, Tanga
WAUMINI
wa Dini ya Kiislamu hapa nchini, wametakiwa kuendeleza umoja, upendo na
mshikamano, katika kuiendeleza dini hiyo ya Mwenyeezimungu.
Ushauri
huo umetolewa na Alhaj Abdul Sharifu kutoka Bagamoyo Mkoa wa Pwani, akitoa
mawaidha katika hafla ya Dhikri iliyofanyika kwenye Msikiti wa Masjid Az Hall
uliopo Kijiji cha Kwenkwale, Halmashauri ya Mkata, Wilaya ya Handeni
mkoani Tanga.
Aidha
Alhaj Sharifu amewaomba viongozi na Waumini wote wa dini hiyo, kukemea vikali
matumizi mabaya ya Dufu yaliyoshamiri maeneo nbalimbali, ambapo alisema kuna
baadhi yao
wanayatumia kwenye ngoma aina ya Viduku.
Wakiongozwa na Mwenyeji wao Alhaj Sheikh Juma na Ma-Alhaj kutoka mikoa mbalimbali waliohudhulia Ziara hiyo, pia Sharifu amewataka waumini hao kurudisha utaratibu uliokuwa unatumiwa na Masheikh ya kutembeleana na kukumbushana mambo yanayoihusu dini hiyo kwani hayo ndio mafundisho ya Mtume Muhammadi Swalallaahu Alayhi Wasalam.
"Waislamu
wenzangu kwenye miaka ya hivi karibuni dini yetu inapoteza mwelekeo, inatupasa
viongozi tusimame imara katika kuhakikisha dini yetu inarejea katika mstari
wake, kuna mtindo unazidi kushika kasi wa dufu kutumika kwenye ngoma ya
Viduku," alisema Alhaj Sharifu.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Alhaj Juma aliwashukuru Ma-Alhaj, Mashehe na waumini wote
kutoka maeneo tofauti waliohudhulia, huku akisema kwamba wamekuwa katika harakati
kubwa za kuiendeleza dini, huku akitoa nasaha kwa vijana kutojiingiza katika
mambo ya kidunia.
"Masheikh
pamoja na juhudi tunazozifanya za kuipogania dini yetu, tunapaswa kuiendeleza
umoja, upendo na mshikamano, pamoja na kuhakikisha vijana wetu wanafuata
misingi imara ya dini ya kiislamu," alisema Alhaj Juma.
Waumini
hao kutoka mikoa mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Tanga, wameshiriki hafla ya Dhikri
hiyo nwishoni kwa wiki.
Waumini wa dini ya
kiislamu wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika msikiti wa Az hall, uliopo Kijiji cha Kwenkwale, Halmashauri ya Mkata, Wilaya ya Handeni
mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment