
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) imeiingizia Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
zaidi ya Tshs Bilioni 3.3 kwa Mauzo ya Miti aina ya Misaji (Teak) kutoka katika
Shamba la Miti Longuza yenye jumla ya Mita za ujazo 4,912.616.
TFS kwa niaba ya Serikali inasimamia Mashamba 23
ya kupandwa kati yake 13 ndiyo yamefikia viwango vya kuvunwa na mashamba mawili
yanavunwa miti aina ya Misaji wakati yanayobaki huvunwa miti aina ya
Misindano,mikaratusi na miti ubani (Cyprus).
Aidha, TFS husimamia pia Misitu ya Asili zaidi ya
500 huku iko hakikisha uzalishaji na usambazaji wa Mbegu bora za Miti unafanya
mwa Nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Wanunuzi, Bwana Ashok
Shanghavi ameuopongeza uongozi wa Shamba la Miti Longuza kwa namna wanavyosimamia
Miti yao
kitaalam kupelekea ubora wa Miti unaoridhisha wafanyabiashara .
Bwana Ashok ameuomba Uongozi wa TFS Makao Makuu
kuhakikisha mashamba yao
yote yanajifunza na kusambaza ujuzi huo ili kuwa na ubora unaofanana kwenye
Mashamba yote.

No comments:
Post a Comment