Naibu Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akiwaonyesha mtambo maalum wa
kuchemsha korosho wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele.
Wataalam hao wametembelea eneo la SIDO kujiridhisha kama
linafaa kwa ajili ya kuanza kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali.
Kaimu
Meneja wa SIDO mkoa wa Mtwara, Zamla Dongwala, akimuonyesha mashine ya kukausha
korosho Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji (hayupo pichani) wakati
alipotembelea eneo la SIDO, mkoani Mtwara leo. Eneo hilo ni moja ya maeneo yaliyochaguliwa kuanza
kutumiwa wa wabanguaji wa korosho wadogo kubangua korosho zilizonunuliwa na
serikali.
Fundi umeme akiwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha matengenezo ya mashine ya kuchambua korosho kama alivyokutwa na mpiga picha wetu eneo la SIDO mjini Mtwara (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment