Na
Omary Mngindo, Makurunge Bagamoyo
WAKAZI
wa Kitongoji cha Gama Makaani, Kata ya Makurunge Bagamoyo Mkoa wa Pwani,
waliomo ndani ya eneo la mradi wa Bagamoyo Sugar, wanamuomba Waziri William
Lukuvi afike kusikiliza kilio chao.
Wakizungumza
na waandishi wa habari kitongojini hapo, wakazi hao walisema kuwa, wanamtaka
Waziri huyo ili wampatie kilio chao, kilichodumu kwa miaka zaidi ya mitano
sasa, huku kukikosekana majibu ya uhakika.
Wakijitambulisha
kwa majina ya Samwel Almass, Hassani Lungwa, Shufaa Nyakoki na Halima Kiongole,
kwa niaba ya wenzao walisema kuwa, kwenye eneo lao awali waliingia makubaliano
na kampuni EccoEnergy ambayo walikubaliana kuwapatia viwanja sanjali na kuwajengea
nyumba.
"Lakini
baadae Serikali ikavunja mkataba na EccoEnergy ikakabidhiwa eneo hili Kampuni
ya Bagamoyo Sugar, wakati wa Kampuni ya awali ikifanya tathimini, wengine
hatukufikiwa kwa kuwa kipindi kilikuwa cha mvua, wengi wetu hatukufikiwa na zoezi
hilo," alisema Lungwa.
Nae
Shufaa alisema kwamba wiki iliyopita walifika viongozi kutika ngazi ya
halmashauri wakawaambia wahame maramoja wapishe mradi huo, huku wengine wakidai
kwamba hawajapitiwa na zoezi la tathmini.
"Kinachoendelea
hivi sasa ni vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi, wanatuambia tuvunje nyumba
tupishe mradi, sisi wengine hatujapitiwa naa tathmini sasa tutakwenda wapi?
alihoji Shufaa.
Shufaa
aliongeza kwamba hivi karibuni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Haji
Abuu Jumaa, Mwenyekiti wa chama hicho Bagamoyo Abdul Sharifu na viongozi
wengine, walifika wakaahidi kufuatilia suala hilo, hivyo wanasubiri majibu
lakini wanashangaa kutakiwa waondoke .ara moja.
Nilipomtafuta
MNEC Haji alisema kuwa katika mkutano uliofanyika kijijini hapo hivi karibuni
baada ya kupokea kutoka kwa wananchi hao wametoa kauli kwamba waliolipwa
wapishe mradi, kwa ambapo hawajalipwa wasubiri malipo yao.
Nilimtafuta
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Fatuma Latu atolee ufafanuzi kuhusu suala
hilo, alijibu kwa mkato tu kwamba hana neno la kuzungunza juu ya suala hilo
No comments:
Post a Comment