UCHAGUZI wa Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam,
umefanyika Desemba 07, 2018 ambapo wajumbe wa Baraza hilo wamekubaliana kwa kauli moja kuwa na
Manaibu wawili kutoka Chama Cha Wananchi CUF na mwingine Chama Cha
Chamapinduzi CCM.
Hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa idadi sawa ya
wajumbe kwa pande zote mbili ambapo Ukawa ulikuwa na wajumbe 12 huku CCM ikiwa
na wajumbe 12.
Akizungumza wakati wakutangaza uamuzi huo
ulioafikiwa na wajumbe wa Baraza hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar
es Salaam, Isaya Mwita alisema kuwa kutokana na hali hiyo kila mmoja
ataongoza kwa kipindi cha miezi mitatu hadi Juni 30 mwaka 2019.
Meya Mwita alieleza wajumbe wa baraza hilo kuwa,
wamefikia uamuzi huo kwani viongozi wamechaguliwa kwa ajili ya kuleta maendeleo
ya waanchi bila kujali vyama vyao.
Alisema kuwepo kwa viongozi wa vyama viwili
tofauti haita wakosesha wananchi maendeleo kwakuwa wote wamechaguliwa kwa
lengo la kuwatumikia wakazi wa jijini hapa.
Meya Mwita alitumia nafai hiyo
kuwasihi manaibu hao walioteuliwa kuonyesha ushirikiano mkubwa kwa ajili
ya kuleta maendeleo jijini hapa kwakuweka itikadi ya vyama vyao pembeni.
“ Ndani ya ofisi hii kupata wasaidizi kutoka vyama
tofauti sio dhambi, lengo langu ni kulifikisha jiji sehemu ambayo inatakiwa,
ninaimani kuwa walioteuliwa leo tutasaidiana bila kujali itikadi za vyama
vyetu” alisema Meya Mwita.
Kabla ya kufanyika kwa maamuzi hayo, Meya wa
Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sita alitoa hoja baada ya kuwepo kwa mvutano
mkali kuwa baraza lijigeuze kamati ili kufanya maamuzi ambayo yatakuwa na
maslahi kwa wananchi kuliko kuendelea na mabishano.
“ Ndugu mwenyekiti hakuna haja ya kuendelea
kubishana ,wote hapa tunafanya kazi kwa ajili ya wanachi wa jiji hili hapa, ningeshauri
tujigeuze kamati ili kufikia muafa wa jambo hili.
Baada ya hoja hiyo kutolewa, wajumbe wa
baraza hilo walikubaliana kuwa kamati ambapo baada ya nusu saa, walirudi kuwa
baraza na hivyo Meya Mwita kutoa maamuzi ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huo umefanyika ikiwa ni baada ya
aliyekuwa Naibu Meya Mussa Kafana kujiuzulu nafasi yake na kujiunga na CCM
Septemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment