Na hadija Hassan Lindi.
Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Lindi, imetoa onyo kwa wananchi,na
watumishi wa mkoa huo walio na tabia ya kupeleka Malalamiko Ofisini kwao kisha
kukataa kutoa ushahidi wa kumtetea Mhalifu.
Onyo hilo limetolewa na kamanda wa Takukuru mkoani
hapa Steveni Chami Jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari
Ofisini kwake.
Chami ametoa onyo hilo
,kufuatia watumishi watatu wa Idara ya Afya Katika kituo cha Afya cha Manispaa
ya Lindi ,kufika Ofisi ya Taasisi hiyo kulalamikia aliyewahi kuwa Kaimu Mganga
Mkuu wa Manispaa hiyo,Abirahi Rashid Mbingu,kudaiwa kudhurumu fedha za
malipo kwa Manesi waliokuwa wamefanya kazi ya ziada.
Alisema kufuatia taarifa
hiyo,waliifanyia kazi ikiwemo kukusanya nyaraka zilizotumika kufanyia
malipo,kuwaita wale watumishi waliodaiwa kulipwa fedha hizo,ili kutambua iwapo
sahihi zilizokuwa zimeonekana ni za kwao na kuzikataa kwamba sio zao na
hawajawahi kulipwa.
Chami alisema baada ya
taratibu zote za ki-Ofisi kukamilika,mtuhumiwa Mbingu Juni 15/2017,alifikishwa
Mahakama ya Wilaya ya Lindi kwa kesi Namba 57/2017,kujibu Shitaka
linalomkabiri, lakini ilipofika zamu ya watumishi hao kutoa ushahidi
wao,waligeuka na kumtetea mshitakiwa.
“Hawa watumishi ambao hapo
awali waliiambia Takukuru hawakuwa wamelipwa fedha za On-Call allowance
zilizoonyesha katika orodha ya walipwaji sio zao,lakini walipofika Mahakamani
waligeuka na kudai sahihi sio zao fedha wamepata”Alisema Chami.
Aidha kamanda chami
amewataja watumishi hao ambao wote amedai ni manesi wa Kituo cha Afya cha
Manispaa hiyo kuwa ni,Stephen Haji,Mwanahawa Swalehe na Mayila Chikamtenda.
“Ugeugeu uliofanywa na
watumishi hawa,kwa makusudi wameamua kumsaidia mtuhumiwa kwa kusema uongo
Mahakamani,kitendo ambacho ni kosa la jinai na kinyume na Kifungu cha 102 cha
Sheria ya kanuni ya adhabu,Sura ya 16/2002”Alisema Chami.
Alisema kutokana na
ugeugeu ulionyeshwa na watumishi hao,Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa
Lindi,Liliani Lugalabamo alilazimika kumuachia huru mshitakiwa Abirahi Rashidi
Mbingu,baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani.
Hata hivyo,Chami alisema
kutokana na kitendo hicho Ofisi ya Takukuru Mkoani Lindi,imewafungulia kesi ya
jinai namba 122/2018,watumishi hao watatu kwa kosa la kusema uongo na kukataa
kueleza ukweli Mahakamani.
No comments:
Post a Comment