Baadhi ya wakulima katika
bonde la Ruvu, kijiji cha Ruvu Darajani kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze
wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wakionesha miche ya mipapai iliyokatwa katwa
katika mashamba yao, PICHA NA OMARY MNGINDO.
...........................................................
Na
Omary Mngindo, Ruvu
WAKULIMA
katika Kijiji cha Ruvu Darajani, Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilaya
ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameiomba Serikali kuingilia kati vitendo
vinavyofanywa na watu wanaojiita wanatoka ofisi inayosimamia bonde la Ruvu
wilayani humo, kwa kufyeka mazao waliyoyapanda.
Wakizungumza
na waandishi wa habari katika mashamba yao, wakazi wakijitambilisha kwa majina
ya Ally Jeki, Zaynabu Kikande Shayo, Ally Jeki na Said Swaiba,
walisema kuwa mwishoni mwa wiki wamevamiwa na watu hao waliokatakata mazao
kwenye mashamba yao.
Swaiba alisema
kuwa siku ya tukio watu hao walipofika waliwachuku vijana wakaelekea nao kwenye
mashamba hayo, kisha kuanza zoezi la kukata mazao pasipokushirikisha viongozi
wa Kijiji, kitendo walichokieleza ni cha uonevu, huku wakiomba serikali ikemee
jambo hilo.
"Tunalima
bustani nje ya mita 60 wanaodai ni mali yao, lakini cha kusikitisha hivi
karibuni wamekuja kuivamia, wamekata mazao yetu ambayo wengi wetu tunayategemea
kuendesha familia zetu, wengine tunasomesha kupitia kilimo hiki," alisema
Swaiba.
Nae
Samir Shayo alilalamika mipapainyake kukatwa baa watu hao ambao walipofika
waliambatana na askari waliokuwa na silaha za moto, kitendo
kilichowaogopesha wananchi hao.
"Kama
mnavyoona, shamba langu lipo mbali na mita za 60 lakini hata kama wamechukua
mita 100 bado wsingefika hapa, lakini wameamua kutufanya kitendo
kibayabsana, tunaomba serikali ikemee vitendo hivi vya kibabe,"
alisema Samir.
Kwa
upande wake Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Ruvu Ramadhani Natamani alisema
kwamba mwezi wa nne mwaka huu walifika ofisini kwao wakawaeleza wanataka kuweka
mipaka ya kuonesha mwisho wa kulimwa, lakini hawakuonekana tena
"Cha
kusikitisha Mtendaji wa Kijiji alipotaka kuwasogelea wajue kinachoendelea,
aliambiwa asiwasogelee eneo walilokuwa wanakata mazao ya wakulima,
tunaomba uongozi wa Mkoa uingiliekati suala hili, " alisema Mnyamani.
Sehemu ya miche ya mipapai
iliyokatwa katwa katika mashamba ya wakulima wa bonde la Ruvu kijiji cha Ruvu Darajani kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze
wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, PICHA NA OMARY MNGINDO.
No comments:
Post a Comment