Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akipokea cheti cha ushiriki wa michezo ya
Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Naibu Spika
wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ambae ni kiongozi wa msafara wa wanamichezo wa timu
ya michezo ya Bunge katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki yaliyofanyika Bujumbura, Burundi katika tukio lililofanyika tarehe 10 Desemba, 2018 katika uwanja wa ndege Mjini Dodoma.
Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akimpongeza Naibu Spika wa Bunge,
Dkt. Tulia Ackson alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma akitokea Bujumbura, Burundi
katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Naibu Spika aliongoza msafara wa timu ya michezo ya Bunge. Kushoto ni katibu wa
Bunge, Mhe. Stephen kagaigai.
Wanamichezo
wa timu ya michezo ya Bunge wakipokelewa na uongozi wa Bunge, watumishi wa
Bunge wakiongozwa na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai walipowasili katika uwanja
wa ndege wa Dodoma wakitokea katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Bujumbura, Burundi.
Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye koti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na
wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge walioongozwa na Naibu Spika wa Bunge,
Dkt. Tulia Ackson (mwenye tisheti nyeusi) baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Mjini Dodoma wakitokea Bujumbura,
Burundi katika
michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naibu
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na wanamichezo wa timu
ya michezo ya Bunge na watumishi wa Ofisi ya Bunge leo tarehe 10 Desemba, 2018
katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, wakati timu hiyo ilipowasili kutoka
Bujumbura, Burundi katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Ikiwa ni kuwaeleza kwa ufupi mafanikio waliyoyapata katika
mashindano hayo na ushirikiano ulioonyeshwa na watumishi wa ofisi ya Bunge
kabla na baada ya mashindano
No comments:
Post a Comment