Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea
na Wananchi wakati akifanya uhamasishaji kwa Wananchi kujiunga na mfuko wa Bima
ya Afya katika mji wa Kitangali Wilaya Newala Mkoa wa Mtwara.
............................................
Na WAMJW-NEWALA, MTWARA
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza
Mangosongo, Kumchunguza Afisa Afya wa Wilaya hiyo maarufu kwa jina la Mama
Flora kwa tuhuma ya Rushwa aliyochukua kutoka kwa Bw.Shaib Mussa kama adhabu ya
kutupa taka hovyo.
Hayo yamefuatia baada ya Mwananchi
aliyejitambulisha kwa jina na Shaibu Musa kutoa malalamiko yake mbele ya
Mhe.Waziri ya kilipishwa shilingi elfu 50,000 na Bibi Afya huyo mwaka Jana.
Waziri Ummy alisema kuwa Watumishi wa Serikali
hasa wa Sekta ya Afya ni lazima wajiepushe na vitendo vya Rushwa na kuacha
tamaa zinazopelekea kuminywa kwa haki kwa baadhi Wananchi wanaotaka kupata
huduma.
“Namtafuta mmoja ili nimtolee mfano kwa Tanzania
nzima, bahati nzuri Mimi ni Mwanasheria, Kosa LA jinai halina muda, hata kama
ni 2017, tunataka huyu mtu afuatiliwe, achunguzwe kama kweli shilingi 50,000
iliingizwa kwenye Halmashauri au haijaingia, tunataka Mazingira masafi lakini
ile hela iende Serikalini” alisema Waziri Ummy.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga
amesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanza rasmi kampeni ya
uandikishaji ya kijiji kwa kijiji katika Mikoa ya Mtwara na Lindi ili
kuwawezesha wananchi hao kuwa kwenye utaratibu mzuri wa kupata huduma za
matibabu.
Bw. Bernard Konga aliendelea kusema kuwa, Wananchi
wamekuwa wakiingia katika umasikini mkubwa kwa kulazimika kuuza mali za familia
kwa lengo la kupata fedha za kugharamia huduma za matibabu.
“Nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri na wananchi wote
walioko hapa, timu yangu inaanza rasmi kampeni ya kijiji kwa kijini kuanzia
wiki ijayo kwa lengo la kumfikia kila mkulima aliyeko katika Mkoa wa Mtwara na
Lindi ili wananchi hawa wawe kwenye mfumo bora wa kupata huduma za matibabu
wakati wowote, alisema Bw. Konga.
Konga aliendelea kusema kuwa zaidi ya asilimia 80
ya wananchi wote wako kwenye sekta ya kilimo hususan maeneo ya vijijini na kwa
kutambua umuhimu wa kulitunza kiafya kundi hili, Mfuko ulianzisha mpango maalum
unaojulikana kwa jina la Ushirika Afya unaowawezesha kujiunga na huduma za NHIF
kwa gharama nafuu.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya Pamoja na uhamasishaji kwa Wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na Leo hii yupo Wilayani ya Newala.
No comments:
Post a Comment