Na Hadija Hassan, Lindi.
Nyumba {38} yakiwemo
majengo yanayomilikiwa na Serikali yamebomolewa na kuezuliwa mapaa, kutokana
na upepo mkali (Kimbunga) uliojitokeza mwanzoni mwa wiki hii, Wilaya ya Liwale,
Mkoani Lindi,
na kusababisha hasara
ambayo bado haijaweza kufaha mika mara moja.
Habari ambazo
zimethibitishwa na Serikali ya Wilaya hiyo,inaeleza tukio hilo limetokea mchana wa Disemba 03 mwaka
huu,Kata za Nangano na Ngunja.
Wakizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG ,baadhi ya wananchi akiwemo Ashura
Juma,Rehema Yusufu, Hemedi Ally Kindamba na Mohamedi Omari walisema upepo mkali
wa Kimbunga uliovuma siku hiyo,umebomoa baadhi ya majumba pamoja na taasisi za
serikali ikiwemo majengo ya shule na hata ghala la kuhifadhia mazao
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Liwale,Sarah Chiwamba amekiri upepo wa Kimbunga hicho kuharibu
Majengo ya Serikali, nyumba za wananchi, nyumba za watumishi pamoja na vyumba
vya madarasa na Maabara.
Chiwamba amefafanua kwa
kueleza kwamba kati ya Nyumba (38) zilizobomolewa (20) zipo kwenye
ubora,zilizojengwa kwa matofari na kuezekwa kwa Bati,wakati (18) zilizosalia
zimeizuliwa mapaa,kufuatia wananchi kujiwekea utamaduni wa kuezeka kwa Bati
bila ya kupigilia Misumali.
‘’Hizi {18} zimejengwa kwa
kutumia tope na Bati zilizoezekwa hazikupigiliwa Misumali,badala yake uziweka
tu na kukandamizia vipande vya Miti’’Alisema Chiwamba.
Aidha,ameeleza Kimbunga
hicho pia kimeezua paa za vyumba viwili vya Maabara Shule za Sekondari za
Nangano na Ngunja, Nyumba mbili zinazotumika kuishi watumishi,Chumba cha Darasa
na Choo kwa Shule ya msingi Nangano,pamoja na Ghala la kuhifadhia Mazao la Kata
ya Nangano.
Aidha Chiwamba alieleza
kuwa kufuatia tukio hilo,zile kaya zilizokumbwa na maafa hayo na kubainika ipo
katika hali isiyo mzuri wamesaidiwa Debe moja la Mahindi kila moja na fedha
kiasi cha Tsh,5,000/-.
Na kuongeza kuwa kwa
waliathirika zaidi wamepatiwa msaada wa kupatiwa Debe moja-moja la Mahindi na
hela kiasi cha Tsh,5,000/-wakati uongozi wa wilaya ukiendelea na taratibu
zingine za kuwasaidia wananchi hao.
Hata hivyo Chiwamba
Alisema kuwa thamani ya nyumba hizo hazijafahamika.
‘’Kuhusu kiwango cha
hasara kilichopatikana naomba tuwasiliane baada ya siku mbili kupita,kwani
wataalamu kwa sasa wapo huko wakitathimini kwanza’’Alisema Chiwamba.
No comments:
Post a Comment