Na Hadija Hassan, Lindi
Radi iliyoambatana na
kiasi kichache cha Mvua iliyonyesha mwanzoni mwa wiki hii, Wilaya ya
Liwale, Mkoani Lindi, imemuuwa mkazi mmoja wa Kijiji cha Mbuli, Kata ya
Kichonda, Salima Kakole {42}.
Habari za uhakika kutoka
Kijijini huko na kuthibitishwa na uongozi wa Serikali ya wilaya hiyo,imeeleza
kwamba Kalole ameuwawa na Radi hiyo,Disemba 03 mwaka huu, majira ya saa 7-8
mchana.
Baadhi ya mashahidi wa
tukio hilo akiwemo Juma Selema, Kindamba Hemedi na Mwajuma
Issaya,walisema kuwa siku ya tukio hill Mvua ndogondogo iliyonyesha ndipo Radi
kali iliweza kujitokeza na kumfika Salima Kalole.
Walieleza kwamba wakati
Mvua hiyo ikinyesha, Salima Kalole alikuwa amesimama nje ya Nyumba yake huko
mashambani, akiendelea kutekeleza majukumu ya kazi zake ndogondogo.
“Mama huyu alikuwa
akizifanya kazi zake ndogondogo nje ya Nyumba yake (uwanjani), hivyo Radi
ilipopiga ilimfika yeye kisha kumuunguza Hali iliyopelekea kupoteza
Uhai wake Papo happy ”Walieleza Mashuhuda hao.
Mashuhuda hao alieleza
kwamba mwanamke huyo ameacha watoto watatu,wakiwemo wanawake wawili na mwanaume
mmoja,mwili wake umezikwa juzi,Disemba 04 mwaka huu,saa 4:0 asubuhi.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo ya
Liwale,Sarah Chiwamba,amekili kuuwawa mwanamke huyo kwa Radi iliyokuwa
imeambatana na kiasi kidogo cha Mvua iliyokuwa inanyesha kwa siku hiyo.
Chiwamba pia amewaomba
wananchi kujiepusha na utamaduni wa kukaa nje,ikiwemo karibu na Miti au
uwanjani pale Mvua zinapoendelea kunyesha na badala yake,wawe wanajihifadhi
kwenye Nyuumba zao.
No comments:
Post a Comment