Mwenyekiti wa Kamati ya
kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka
akikagua barabara ili kujiridhisha na ubora wake, Kamati hiyo ilipotembelea
na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara Kuu ya kutoka Afrika Kusini mpaka
Misri kipande cha Dodoma – Iringa Kilomita 260 maeneo ya Mlowa mkoani
Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mwenyekiti wa Kamati ya
kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka
akiwaongoza wajumbe wa Kamati hiyo kukagua barabara maeneo ya Mlowa Mkoani
Dodoma ili kujiridhisha na ubora wake, Kamati hiyo ilipokagua mradi wa ujenzi
wa barabara kuu kutoka Afrika Kusini mpaka Misri kipande cha Dodoma – Iringa
Kilomita 260 hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda akiuliza jambo
kwa Mkurugenzi wa barabara Mhandisi John Ngowi (wa kwanza kushoto), Kamati hiyo
ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Iringa
Kilomita 260 maeneo ya Mlowa hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi Selemani Kakoso, akisisitiza jambo
kwa Naibu Mawaziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias
Kwandikwa na Mhe. Atashasta Nditiye, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa
Kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Selemani Kakoso.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege
cha Dodoma, Bi. Bertha Bankwa, akielezea mkakati wa uboreshaji wa kiwanja hicho
kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokikagua.
Muonekano wa barabara ya kuruka na kutua ndege
katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. Barabara hiyo imerefushwa kutoka mita
2,000 hadi mita 2,500.
Mhandisi Kedrick Chawe kutoka Wakala wa
Barabara (TANROADS), akionesha ramani ya Kiwanja cha Ndege cha Msalato
kitakavyokuwa mara baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi wake kukamilika kwa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua eneo
ambalo kiwanja hicho kitajengwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga,
akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260) kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Ofisi za Bunge
jijini Dodoma, leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka, akikagua ubora
wa lami katika eneo la Nkulabi, barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260), wakati
kamati hiyo ilipokagua barabara hiyo leo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara kutoka Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi John Ngowi,
akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), walipokagua barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260).
Muonekano wa Barabara ya
Iringa -Dodoma (Km 260) sehemu ya Migori- Fufu (Km 93.80) ambayo ujenzi wake
umekamilika kwa kiwango cha lami.
No comments:
Post a Comment