Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza
jambo wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika
Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.
.............................
Na
WAMJW-DOM.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanukiwa kuokoa kiasi cha Shilingi Bilion
3.4 ambacho kingetumika katika matibabu kwa Wagonjwa wa Figo nje ya Nchi.
Dkt.
Ndugulile ameyasema hayo leo Machi 14 wakati akiongea na Waandishi wa Habari
katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma ikiwa ni Siku ya Figo Duniani
ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Afya ya figo kwa kila mmoja kila.
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho
kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya
nchi kwaajili ya matibabu.
“Wagonjwa
waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka wagonjwa
nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo
ya wagonjwa. 80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi
cha shilingingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” Alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha, Dkt,
Ndugulile amesema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia magonjwa ya figo ni
pamoja na uzito wa kupindukia (obesity), matumizi makubwa ya sigara, unywaji wa
pombe, uvutaji wa sigara,kutokufanya mazoezi na kunywa madawa kiholela hasa
dawa za kupunguza maumivu.
Aliendelea
kusema kuwa, magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu ni magonjwa yanayoongoza
kwa kusababisha matatizo ya figo, magonjwa haya yakitambuliwa mapema yanaweza
kudhibitiwa kwa matibabu na kuepusha madhara kwenye figo.
Kwa upande
mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Kufikia Desemba mwaka 2018, jumla ya vituo
28 vyenye jumla ya wagonjwa 1050 vilikuwa vikitoa huduma ya usafishaji damu
katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma.
Mbali na
hayo, Dkt. Ndugulile amesema Serikali imepiga hatua kubwa ya kuanzisha huduma
za kupandikiza figo hapa nchini katika hospitali ya Taifa Muhimbili na
Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Figo nchini Dkt. Onesmo Kisanga
amesema kuwa Ugonjwa wa Figo ni tatizo kubwa nchini huku wananchi wengi wakiwa
na uelewa mdogo juu ya athari na visababishi vya ugonjwa huo.
Aidha Dkt.
Onesmo amewataka wananchi kuacha tabia ya kunywa dawa bila kupata ushauri wa
kitaalamu hivyo kuepuka kuzalisha sumu mwilini na kupelekea ugonjwa wa figo.
Hata hivyo
Dkt. Onesmo Kisanga ameishukuru Serikali kwa kuwaendeleza kimasomo wataalam
kwenye upande wa matibabu ya figo ambao sasa wamesambazwa sehemu mbali mbali
ndani ya nchi kutoa huduma za matibabu.
Naye Dkt.
Grace Maghembe Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya amesema ungojwa
huu umekuwa ukiwaathiri zaidi wakazi wa mijini kuliko vijijini kutoka na mfumo
wa maisha uliopo sasa ambapo watu wengi wamekuwa hawazingatii mtindo bora wa
maisha kwa kutofanya mazoezi pamoja na kula chakula bora.
Dkt.
Maghembe amesema bado ipo changamoto kwenye matumizi ya dawa za mitishamba
ambazo bado hazijatambuliwa na kuthibitishwa huku akiwataka wananchi kuwa
waangalifu pia kwenye matumizi ya dawa hizo.
“Serikali
inatambua umuhimu wa tiba mbadala pamoja na matibabu ya tiba za asili na ndio
maana zipo taasisi za serikali zinazohusika kuzitambua dawa hizo ni zipi na
zina vitu gani na unatakiwa kutumia kwa kiwango gani” amesema Dkt Maghembe
nakuwataka watengenezaji wa dawa hizo kufuata taratibu zilizopo ili
kuthibitisha na kusajili dawa zao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari
(Hawapo kwenye picha) wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa
leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe na wamwisho ni Mwenyekiti
wa Chama cha Magonjwa ya Figo nchini Dkt. Kisanga
Waandishi wa Habari waliojitokeza kumsikiliza
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika
Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment