RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu na jamaa, kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, kilichotokea leo, tarehe 21 Septemba 2026.


Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa, akieleza kuwa anaungana na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi.


Amesema Marehemu Mama Fatma Karume amekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania, akiwa mwenza wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar.


Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe na amrehemu Marehemu Mama Fatma Karume na amjaalie makaazi mema Peponi, pamoja na kuipa familia subira katika kipindi hiki kigumu.



Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU