Wednesday, March 27, 2019

MWAKYEMBE AISHAURI NMB KUONGEZA VIWANGO VYA MIKOPO.

 Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Dkt Halison Mwakyembe, (kulia) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya kusini, Janeth Shango (kulia)alipotembelea katika banda la maonyesho la Benk hiyo katika kongamano la  jukwaa la fursa za Biashara na uwekezaji za Mkoa wa  Lindi lililofanyika Manispaa ya Lindi Mkoani Humo 
.............................................. 

NA HADIJA HASSAN, LINDI

Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Dkt Halison Mwakyembe ameishauri Benki ya National Microfinance Bank (NMB) Kuongeza kiwango cha mikopo wanayoitoa  ili kuwapa fursa Wananchi wengi kukopa


Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jana alipotembelea katika banda la maonyesho la Benk hiyo katika kongamano la  jukwaa la fursa za Biashara na uwekezaji za Mkoa wa  Lindi lililofanyika Manispaa ya Lindi Mkoani Humo 


Mwakyembe alisema pamoja na Bank hiyo kujikita katika kutoa Mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali, wafanya biashara  na wakulima ni vyema wakaona umuhimu wa kuongeza kiwango cha fedha wanazozitoa kwa wafanya biashara hasa katika Mkoa wa Lindi ili uwekezaji uweze kuleta tija


"Baada ya jukwaa hili tengeni fedha za kutosha zaidi kwani baada ya jukwaa hili la fursa za Biashara kufunguliwa bira shaka wafanya biashara watapenda kukopa ili waweze kuwekeza" alisema Waziri Mwakyembe


Awali akitoa maelezo mbele ya Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Dkt Halison Mwakyembe afisa mahusiano wa Banki hiyo Janeth Shango Alisema kuwa wao kama Benki ya NMB kwa kuzingatia fursa zilizopo Nchini wanaungana na Serikali kuhakikisha wanasaidiana katika kuhakikisha Wakulima wote wanafikia fursa wanazoziona katika mikoa yao


Alisema katika kukamilisha adhima hiyo kwa kipindi cha miaka mitano2015/2020 Bank yao  imetenga kiasi cha sh.Bilioni 500 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima kote Nchini ambapo mpaka sasa tayari sh. Bilioni 450 zimeshatolewa kwa wakulima moja moja na kwa vikumdi


Aidha alisema kuwa pamoja na kutoa Mikopo hiyo kwa wakulima wadogo, wakubwa na wakati lakini pia Mikopo hiyo inatolewa kwa wafanya biashara wanaohusika na usafirishaji wa mazao hiyo ni kwa kuwa wametambua kuwa kilimo ndio uti wa mgongo kwa Nchi

No comments:

Post a Comment