Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Kangi Lugolawa Mamb
………………………………………
Na Felix
Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelazimika kuwasili kwa mara nyingine
Mkoani Morogoro leo, kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imeibua
mifarakano baina ya wananchi Mkoani humo.
Waziri
Lugola, wiki iliyopita alimaliza ziara yake Mkoani humo iliyokuwa na lengo la
kusikiliza kero mbalimbali za wananchi kuhusiana na utendaji kazi wa Taasisi za
Wizara yake.
Lugola
katika ziara yake Mkoani humo, alifanya mikutano ya hadhara ambapo alikutana na
migogoro mbalimbali lakini kero kubwa kati ya hizo ni kuhusiana na ardhi ambayo
inapelekea wananchi kuwekeana chuki, kujeruhiana, kufikishana Polisi pamoja na
kuuana.
Kati ya
Wilaya tatu alizozitembelea alipokuwa Mkoani humo, ni Morogoro, Mvomero na
Kilosa, licha ya wananchi kutoa kero zao mbalimbali, mgogoro wa ardhi uliibuka
kwa sehemu kubwa hasa katika Wilaya ya KIlosa.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii, Waziri Lugola alisema alipokuwa Wilaya ya Kilosa,
alikutana na mgogoro wa ardhi ambapo umeleta mgawanyiko miongoni mwananchi
hivyo akawaahidi kurejea tena Wilayani humo kwa ajili ya kutatua kero zao baada
ya kukutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Lugola
alisema mipango yote ipo sawa, hivyo anatarajia kufanya mkutano wa hadhara na
wananchi wa Kilosa Kesho Machi 15 Wilayani humo ili kuwapa majibu ya kero zao
pamoja na kumaliza mgogoro wa ardhi unaowakabili.
“Migogoro
mingi inaletwa vituo vya polisi hasa Wilaya ya Kilosa, na wananchi katika
mikutano yangu ya hadhara wanalalamika kuhusiana na ardhi, baadhi wanawalaumu
polisi wangu kutokuwatendea haki na wengine pia wanawapongeza kwa kazi nzuri,
na wengi wao wanalalamikia kuwa matajiri ndio wananyang’anya ardhi zao
wakitumia fedha kwa wakiwahonga Polisi,” alisema Lugola.
Aliongeza
kuwa, alipokuwa katika mkutano wake wa mwisho katika Tarafa ya Kimamba, Wilaya
ya Kilosa Mkoani humo, kuliibuka na hoja nyingi za migogoro ya ardhi, kutokana
na usugu wa tatizo hilo, aliwaahidi wananchi wa Wilaya hiyo atarejea tena kwa
ajili ya kutatua mgogoro huo.
“Ziara
yangu niliikatisha katika Mkoa huo, kwa ajili ya kwenda Dar es Salaam
kuhudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri, hata hivyo, niliwaahidi wananchi
nitakutana na Waziri wa Ardhi, ili tushirikiane kutatua mgogoro huu ambao
unaweza ukaleta vurugu kubwa pale Kilosa na Mkoa wa Morogoro kwa ujumla,”
alisema Lugola.
Lugola
anatarajia kufanya mkutano mwingine wa hadhara kuleta majibu ya ahadi
alizowaahidi wananchi hao pamoja na kusuluhisha mgogoro huo ili wananchi
waendelee kufanya shughuli zao za maendeleo kama kawaida.
Waziri huyo
alisema, hawezi kukaa ofisini huku wananchi wakiwa wanapata matatizo mitaani,
hivyo atazunguka nchi nzima kuzungumza na wananchi na kupokea kero mbalimbali
zinazowakabili.
“Wananchi
wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio
mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua
matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi
zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Dokta Magufuli
inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na
Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola.
Lugola
alisema Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi
la Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Idara ya Probesheni na Huduma kwa
Jamii, zifanye kazi za kiweledi bila kuwaonea wananchi.
No comments:
Post a Comment