Na EZEKIEL NASHON, DODOMA
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso
amewataka wataalamu wa maji kutumia taaluma zao vizuri, na kuacha tabia ya
kuwadanganya viongozi pindi wanatofuatilia miradi katika maeneo yao ya
kazi kuwa miradi hiyo iko vizuri hali kwamba kuna kasoro katika miradi hiyo.
Aweso ameyasema hayo jana jijini
Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha wadau wa maji, Wakurugenzi,
wakuu wa mamlaka za maji na wenyeviti wa bodi za maji waliokaa kwa siku mbili
Dodoma kupewa uelewa namna ya utekelezaji wa sheria mpya maji na usafi wa
mazingira, pamoja na uanzishwaji wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira
vijijini.
Amesema wataalamu hao wamekuwa
wakitumia taaluma zao vibaya katika nafasi zao na kufikia kipindi kuwadanganya
viongozi kuwa hakuna shida kwenye miradi ya maji mbalimbali, lakini ukifuatilia
kwa undani unakuta kuna matatizo mengi na wananchi hawapati maji.
“Hili limekuwa ni tatizo kubwa kwa
wataalamu wetu kwa sababu tukifika kukagua miradi ya maji tunaambiwa miradi iko
vizuri lakini ikiikagua kwa umakini unakuta kuna matatizo makubwa, tabia hii
muache natumaini kupitia kikao hiki mutakuwa mmejifunza mengi,” amesema.
Amesema hata sita kumfukuza kiongozi
yeyote ndani ya mamlaka hiyo ambaye atakwenda kinyume na maelekezo yao, hata
kama hata kama atakuwa vipi tutamtoa tu, japo hakuna mtu anayependa kumfukuza
mtu katika kazi yake viongozi tunapenda kuwaona mkiwa kazini.
Pia amewataka kulinda taaluma zao
vipaji, ujuzi na maalifa yao kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji kama
makusudio ya serikali yalivyo, amewataka kujidhatiti kuhakikisha wanatatua kero
zilizopo katika sekta hiyo.
Kwa upande wake Barnabas Ndunguru
ambaye ni mkurugenzi wa Idara ya utawala wizara ya maji,aliyekuwa
akimuwakilisha katibu mkuu, amesema watatumia taaluma zao kuhakikisha
wanashirikiana na wizara kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi kwa
ufasaha na hasa katika kutekeleza majukumu ya mamlaka mpya ya maji
na usafi wa mazingira vijijini RUWASA.
Nae afisa maji bonde la ziwa nyasa
Alice Mnali, amesema watahakikisha wanalinda taaluma zao kuhakikisha sekta hiyo
inakuwa na kuleta anufaa katika jamii, na yale yote waliopata katika
mawasilisho mbalimbali watahakikisha wanayatendea kazi, na hawatakuwa kikwazo
katika sekta ya maji.
No comments:
Post a Comment