Sunday, March 31, 2019

RC. NDIKILO AWATOA HOFU BAGAMOYO NA KIBAHA.

 Naomba nichukue fursa hii kuwahakikishia wananchi wa maeneo ya Kibaha na Bagamoyo waliokuwa wanahudumiwa na substation ya Mlandizi iliyopata msukosuko jana wa kuungua moto kwenye moja ya transfoma zake kwamba juhudi zinafanyika ndani ya shirika la TANESCO kufunga transforma nyingine ili nishati ya umeme iendelee kupatikana majumbani kwetu na kwenye maeneo ya uwekezaji vikiwemo viwanda. 


Serikali yetu imejipanga vizuri ili kuhakikisha kwamba tatizo hili halitaathiri shughuli zetu za kila siku za kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa mkoa wetu na nchi yetu kwa ujumla. Hatua za muda mfupi tayari zimeshachukuliwa na shirika la TANESCO ili tuendelee kupata huduma ya nishati ya umeme katika maeneo ya Kibaha na Bagamoyo. 


TANESCO itarejesha tranforma hiyo kubwa kama iliyokuwepo hapo awali ili iendelee kuhudumia viwanda vyetu. Naomba tuwe na subira.

IMETOLEWA NA MKUU WA MKOA WA PWANI
MHANDISI EVARIST NDIKILO.
Image may contain: outdoor

 Hali ilivyokuwa katika kituo cha kupozea umeme cha Mlandizi baada ya moja ya tranforma zake kuungua moto mapema jana Machi 30, 2019.
Image may contain: cloud, sky and outdoor 

Muonekano katika kituo cha kupozea umeme cha Mlandizi baada ya moto kuzimwa kufuatia moja ya tranforma zake kuungua moto mapema jana Machi 30, 2019.

No comments:

Post a Comment