Friday, March 15, 2019

ZAIDI YA WATU 40 WAMEUWAWA MISIKITINI NEW-ZEALAND.

Zaidi ya watu 40 wauwawa kwenye mashambulizi ya misikiti New-Zealand.


Misikiti miwili ya ChristChurch nchini New Zealand imeshambuliwa wakati wa sala ya Ijumaa hii leo. Watu wasiopungua 49 wameuwawa.


Polisi wanasema watu wanne, watatu wanaume na mmoja mwanamke wamekamatwa. Haijulikani kama watuhumiwa ni miongoni mwa waliokamatwa.


Kwa mujibu wa mashahidi bwana mmoja aliingia msikitini na kufyatua risasi, Baadae risasi zilifyatuliwa pia katika msikiti wa pili.


Kanda ya video imesambaa mitandaoni ambapo mtuhumiwa anaonyesha jinsi alivyoshambulia msikiti mmoja kati ya hiyo miwili.


Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amsema watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.


Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa ni shambulio lililotanda 'kiza kikubwa' siku ya leo nchini humo.


Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa kwa kuhusika na shumbulio hilo.


Kamishna wa polisi Mike Bush amesema, kwamba huenda washukiwa zaidi wakakamatwa.


Taarifa kutoka nchini New Zealand kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.


Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

No comments:

Post a Comment