Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo
na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Dkt. Richard Sezibera.
Katika
mazungumzo yao, Mhe. Sezibera alimpongeza Mhe. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mazungumzo hayo
yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe.
Ernest Mangu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo. Mhe. Sezibera yupo
nchini kwa ajili ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene
Kayihura (kulia) na Afisa Ubalozi wa Rwanda wakifuatilia mazungumzo kati ya
Mhe. Prof. Kabudi na Mhe. Dkt. Sezibera (hawapo pichani).
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa
Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Afrika Bw. Wilbroad Kayombo wakiwa kwenye Mazungumzo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo
ya Nje wa Rwanda, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wapili kutoka kushoto) wakiwa
katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini
Rwanda, Mhe. Ernest Mangu (wa kwanza kulia) na Balozi wa Rwanda nchini
Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao.
No comments:
Post a Comment