Na Omary Mngindo, Rufiji
JUMUIA ya Wanawake Mkoa wa Pwani, mwishoni mwa wiki imetembelea na kuukarabati mnara wa kumbukumbu ya Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Bibi Titi Mohamed.
Mnara huo wa kumbukumbu uliojengwa katika Kijiji cha Mkongo, Kata ya Mkongo Tarafa ya Mkongo jimbo la Rufiji mkoani hapa, unataraji kuboreshwa kisha kutangazwa kuwa utalii, ikiwa ni kumtangaza mwanasiasa huyo mkongwe, aliyepigania Uhuru wa nchi na Afrika Mashariki ambapo mnara wake umejengwa kijijini hapo.
Hayo yamebainika katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani inayotaraji kufanyika Machi 8 mwaka huu, ambako Mkoa umekuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea mnara huo ukitanguliwa na zoezi la kutembelea vituo vya watoto waishio kwenye mazingira hatarishi pamoja na wagonjwa.
Akizungumza katika sherehe hiyo, Ramadhani Maneno Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwapongeza wana-UWT hao kwa kuona umuhimu wa kutembelea mnara huo, wa kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kupigania Uhuru, pia Naibu Waziri wa kwanza kutokea mkoani Pwani wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza.
"Nimeridhishwa na maamuzi yenu ya kunipatia heshima ya kuwa mgeni rasmi, kwani mlikuwa na maamuzi ya kumteuwa mwengine yeyote kuja katika hafla hii, niwaombe mtafute jambo lingine litalotujumuisha kama hivi likiwa ni la ngazi ya Mkoa badala ya Kitaifa pekee," alisema Maneno.
Sherehe hiyo ambayo Maneno aliongozwa na Mwenyekiti wa Jumuia husika Farida Mgomi, pia imehudhuliwa na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, wakiwemo wabunge Mohamed Mchengerwa wa Rufiji na Ally Ungando wa Kibiti, pia kulikuwa na kongamano maalumu likijumuisha mada mbalimbali.
Mgomi alisema kuwa chanzo cha kuwepo kwa siku hiyo imetokana na wanawake waliokuwa wanafanyakazi viwandani kukosa muda wa kupumzika, kufungiwa ndani wakati mwingine kulikuwa na joto, pia ujira mdogo.
"Kutokana na hali hiyo ndipo wakaamua kuandamana wakidai haki yao, katika tukio hilo ikatumika nguvu hali iliyosababisha kuuawa kwa wanawake, nchini Marekani, nasi Pwani kwa makusudi kutoka katika nafsi zetu tuneamua kuja katika mnara wa Bibi Titi Mohamed ikiwa ni sehemu ha kuelekea maadhimisho hayo," alisema Mgomi.

Ramadhani Maneno Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani akitoa neno kwa wanaJumuia wa Wanawake mkoani
hapa walipokuwa katika Mnara wa Bibi Titi Mohamed uliopo Kijiji cha Mkongo
wilayani Rufiji. Picha zote na Omary Mngindo.
No comments:
Post a Comment