Mwalimu Respicius Mutazangira ambae amehukumiwa kunyongwa akiongozwa na polisi.
.............................
Mahakama kuu kanda ya Bukoba imemuhuku kumnyonga
hadi kufa Mwalimu Respicius Mutazangira baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga
hadi kumuua Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Kibeta, Sperius
Eradius mwishoni mwa mwaka 2008.
Aidha, mshtakiwa mwenzake Mwalimu Heriet Gerald
ameachiwa huru.
Katika kesi hiyo walimu hao walishitakiwa kwa kosa
la kumuadhibu kwa kipigo Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Kibeta,
Sperius Eradius.
Hukumu hiyo imetolewa leo na jaji Lameck Ml
acha
ambae alisikiliza kesi hiyo kwa muda wa mwezi mmoja.
TUKIO LILIVYOTOKEA KWA UFUPI.
Mwanafunzi huyo alipata adhabu ya kupigwa na kumsababishia kifo chake.
Mwanafunzi huyo inadaiwa alikwenda kumpokea
mizigo mwalimu wake (Heriet Gerald) aliyefika shuleni hapo kwa usafiri wa
bodaboda, lakini baada ya kuingia ofisini alianza kulalamika kutoiona pochi
yake.
Kwa mujibu wa Wanafunzi wenzake, walidai mwanafunzi mwenzao (Sperius Eradius) aliitwa na kuanza kuhojiwa kuhusu kupotea kwa pochi hiyo na akakana kuichukua, hali iliyosababisha kuanza kupigwa akitakiwa kuirejesha.
Walisema kuwa baadaye walitakiwa kuitafuta pochi hiyo mpaka chooni, lakini hawakuiona huku mwanafunzi huyo akiendelea kuadhibiwa.
Hata hivyo, ilielezwa na wanafunzi hao kuwa wakati mwanafunzi mwenzao akiendelea kupigwa, dereva bodaboda alifika shuleni hapo akimtafuta mwalimu aliyepoteza pochi na kumkabidhi pochi aliyokuwa ameisahau kwenye pikipiki yake.
Mashuhuda hao walisema kuwa baada ya pochi hiyo kupatikana, mmoja wa walimu aliagiza mwanafunzi huyo apatiwe juisi na bagia, chakula ambacho hakuweza kukila kutokana na maumivu.
Mwalimu Heriet Gerald ambae ameachiwa huru na mahakama.
No comments:
Post a Comment