- Wamezindua huduma ya mtandaoni ya M-Koba iliyounganishwa na M-Pesa inayotoa fursa ya kuhifadhi fedha kwa usalama na uwazi.
- Inatarajia kuondoa changamoto za upotevu wa fedha na kuimarisha mitaji ya vikundi hivyo.
Dar es Salaam.
Wanachama wa vikundi vya kifedha vya kijamii (Vicoba), vikundi rasmi na
visivyo rasmi maarufu kama ‘upatu’ sasa wamepata suluhu ya kuhifadhi
fedha zao baada ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom kwa
kushirikiana na benki ya Posta Tanzania (TPB) kuzindua huduma ya
mtandaoni inalotoa suluhisho la utunzaji fedha kidijitali.
Huduma
hiyo, iliyopewa jina la M-Koba, iko chini mfumo wa huduma za kifedha
kwa njia ya simu wa M-Pesa, itawezesha vikundi hivyo kutunza fedha
kidijitali kwa usalama na uwazi zaidi.
Kaimu
Mkurugezi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi aliyekuwa
akizungumza katika uzinduzi huo leo (Februari 28, 2019) jijini Dar es
Salaam, amesema huduma hiyo itakuwa endelevu na kukidhi mahitaji ya
vikundi vya kifedha kupata eneo salama la kutunza fedha na kuimarisha
mitaji yao.
"Huduma
hii ya kidijitali inalenga kutoa huduma endelevu ambayo itatumiwa na
kufikia vikundi vilivyopo maeneo mbalimbali nchini kwa njia ya mtandao
mkubwa wa Vodacom, "amesema Hendi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vodacom, inakadiriwa kuwa asilimia 16
ya watanzania (zaidi ya watu milioni 4.4) wengi wao wakiwa wanawake, ni
wanachama wa vikundi zaidi ya 50,000 vya kuweka akiba na mikopo (Vicoba)
ambao huhifadhi akiba zaidi ya Sh100 bilioni kwa mwaka.
Pia
kuna vikundi visivyo rasmi zaidi ya 50,000 visivyo rasmi vya wahitimu
wa vyuo, wafanyakazi na wanafamilia ambao wanatumia mitandao ya kijamii
kuweka akiba na kukopa.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi wa kwanza kulia
akishirikiana na viongozi wengine kuonesha jarida la M-Koba wakati wa
hafla ya kuzindua huduma ya M-Koba, huduma ya kwanza na ya kipekee
nchini kwa ajili ya vikundi vya kuweka akiba nchini
Tanzania.Picha|Vodacom.
Afisa
Mtendaji mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi amesema huduma hiyo inalenga
kuongeza theluthi moja ya idadi ya watu waliosajiliwa katika mifumo
rasmi ya kifedha na zaidi kuwafikia wanawake wa vijijini ambao
wanajihusisha na shughuli hizo.
“Kama
taasisi ya kifedha, tunatambua umuhimu wa vikundi hivi na ndiyo sababu
tumeshirikiana na vinara hawa wa sekta ya simu kuleta suluhisho hili la
kidijitali ambalo litarahisisha kutunza akiba na kuwezesha watu kufikia
malengo yao," amesema Moshingi
Naye
Mwenyekiti wa mojawapo wa Vicoba aliyehudhuria uzinduzi huo, Abdallah
Mkenga amesema huduma hiyo limekuja wakati mwafaka kwa sababu
itawasaidia kutatua changamoto za utunzaji fedha.
“Sasa
tuna mfumo salama zaidi wa vikundi vyetu na tunachanga kwa uwazi kwani
mfumo huu unaruhusu kuonekana kwa shughuli za kikundi," amesema Mkenga.
Kutokana
na umuhimu wake katika jamii, Vicoba vimejumuishwa katika Sheria mpya
ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 ambapo sheria hiyo imeweka
utaratibu wa kuiwezesha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kutoa elimu kwa
watumiaji wa huduma ndogo za fedha hususan vikundi vya kijamii kwa lengo
la kunufaika na fursa zilizopo.
Vicoba,wakopeshaji
binafsi na asasi za kijamii vinaingia katika daraja la nne la sheria
hiyo ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati wa
kupitisha sheria hiyo bungeni mwaka jana alisema vikundi hivyo
viitaandaliwa kanuni na miongozo mahsusi kwa ajili ya kusimamia daraja
hilo.
No comments:
Post a Comment