MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa utabiri wa mvua za masika ambazo
tayari zimeanza kwa baadhi ya mikoa na zitaendelea kunyesha hadi mwaka
huu.
Taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoitolewa leo jijini Dar es
Salaam imesema utabiri wa mvua za masika (MAM) 2019 ni kwamba kuanzia wiki ya
nne ya Februari katika mikoa ya Kagera mvua itanyesha na kusambaa katika mikoa
ya Geita, Mwanza, Shinyanga,Simiyu,Kigoma Kaskazini na Mara wiki ya pili ya
Machi 2019.
Mvua hizo kwa baadhi ya meeneo zitakuwa juu ya wastani hadi wastani na
kwamba mvua za msimu 2018,2019 zinaendelea hadi Aprili mwaka huu.Kwa mujibu wa
TMA ni kwamba mvua zitaisha wiki ya kwanza ya Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment