Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo
cha Uhandisi na Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto), akimkabidhi Katibu wa
Madrasat-ul-Istiqama, Ustaadh Hemed Suleiman misahafu 29, kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka hiyo, Richard Mayongela.
Baadhi ya Wafanyakazi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakishughudia Kaimu Mkurugenzi wa
Kitengo cha Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto)
akikabidhi Katibu wa Madrasa ya Istiqama ya Buguruni, Ghana, Ustaadh Hemed
Suleiman moja ya misahafu 29 waliyotoa msaada.
....................................
Na
Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), leo imetoa vitabu vya dini aina ya
misahafu 29 kwa Madrasat-ul-Istiqama ya Buguruni, Mtaa wa Ghana, kwa ajili ya
watoto wanaosoma elimu ya dini ya Kiislam.
Akikabidhi
vitabu hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi
na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu amesema mbali na kazi za kuendesha,
kusimamia na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania Bara, TAA imekuwa
ikishirikiana na jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii.
Mhandisi
Mdemu amesema pamoja na kwamba Madrasat hiyo ina watoto takribani 230, lakini
anaamini wataweza kupokezana vitabu hivi na kupata mafunzo yaliyo sahihi,
yatakayowajengea malezi bora yenye msingi wa amani na mshikamano.
Amesema
msaada huu wa vitabu vya dini utasaidia kuanza kuwaandaa watoto hao, ambao
baadaye wakiwa wakubwa wanakuwa ni sehemu ya jumuiya na sehemu ya Mamlaka na
jamii nzima ya Kitanzania, ambapo watakuwa waadilifu na wenye maadili mema kwa
taifa kwa kuwa wamepata msingi mzuri wa elimu ya dini, ambao ndio chimbuko la uadilifu
na amani.
“Hii ni
kawaida ya Mamlaka kutoa misaada kwa jamii, na ninaamini msaada huu pia
utasaidia kufanya kitu kikubwa katika jamii yetu, kwa kuwa watoto hawa ndio
watakuja kuwa watumishi wa miaka ijayo, hivyo watakuwa mfano wa kuigwa katika
jamii,” alisema Mhandisi Mdemu.
Pia
Mhandisi, amewakaribisha kutembelea TAA kwa ajili ya kujifunza na kuwa na ari
ya kufanya kazi na Taasisi hii, ambayo ipo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi).
Naye Katibu
wa Madrasat hiyo, Hemed Suleiman ameishukuru TAA kwa kujitoa kwao kwa kutoa
msaada huo, ambao ni moja ya vitu muhimu kwao.
“Nawashukuru
sana tena sana kwa msaada huu, hatuna cha kuwalipa ila Mungu awazidishie pale
mlipotoa, muendelee kuwasaidia watu zaidi ya sisi” ameshukuru Bw. Suleiman.
No comments:
Post a Comment