Wednesday, March 27, 2019

VETA KUANZA KUTUMIA KISWAHILI KUFUNDISHIA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, sayansi na teknologia Dokta Avemaria Semakufu amevitaka vyuo vya  ufundi stadi  kupunguza vigezo vya udahili wa wanafunzi  kujiunga katika vyuo hivyo ili kuwawezesha wahitimu wa darasa la saba kupata elimu na mafunzo ya ujuzi mbalimbali.


Dokta Semakafu  ametoa wito huo wakati wa warsha ya makabidhiano ya mitaala na mihtasari ya m mafunzo ya elimu ya ufundi stadi iliyotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili ambapo amesema  vijana wengi wapo mitaani  na wanapenda kujiunga na vyuo vya ufundi (VETA)lakini  wanashindwa kutokana na masharti  kuwa magumu.


Aidha   Naibu katibu mkuu huyo amesema  kuwa kupatikana kwa mitaala ya Kiswahili katika vyuo vya ufundi kutasaidia kuongeza kasi ya nchi kwenda uchumi wa viwanda pamoja na uchumi wa kati  huku mkuu Mkurugenzi Mkuu vyuo vyamafunzo na  ufundi stadi (VETA) Dokta Pancras Bujulu  akabainisha mabadiliko ya mitaala  itakavyosaidia  katika ongezeko la udahili wanafunzi pamoja na  wataalamu nchi.


Kwa  upande wake  Dokta Annastella Sigwejo Kutoka Baraza la Taifa Elimu ya Ufundi  akabainisha lengo la mabadiliko ya mitaala hiyo kuwa ni kwasaidia watanzania ambao hawajabahatika kufika elimu ya sekondari huku mkufunzi wa chuo cha maendeleo ya wananachi  Msingisi Cha mkoani Singida  Bw. John Well Well ameishukuru serikali kufanya mabadiliko hayo kwani itawasaidia katika ufundishaji.


Warsha hiyo imehusisha wakufunzi kutoka vyuo vya maendeleo wananchi na wakuu wa vyuo vya ufundi Stadi .

No comments:

Post a Comment