Kiongozi Mwandamizi wa Dar es Salaam Nature Study, Mwalimu, Yasini Mkwizu akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG katika kituo hicho.
Kiongozi Mwandamizi wa Dar es Salaam Nature Study, Mwalimu, Yasini Mkwizu (katikati) akiongoza msafara wa wanafunzi pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Aljebra ambao walifanya ziara ya kimasomo katika eneo hilo.
Kiongozi Mwandamizi wa Dar es Salaam Nature Study, Mwalimu, Yasini Mkwizu (katikati) akiongoza msafara wa wanafunzi pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Aljebra ambao walifanya ziara ya kimasomo katika eneo hilo.
..............................
Kituo cha Dar es Salaam Nature study kilichopo
eneo la Nyebulu Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, ni kituo cha elimu kwa
vitendo ambapo wanafunzi wa ngazi mbalimbali hujionea vitu kwa uhalisia wake na
kujifunza katika masomo ya Kilimo, Jiografia, Sayansi, na utunzaji wa mazingira
ambapo katika kukua kwa miji hutokea tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira.
Mwalimu Mng'ala Abdallaah Mtegetwa ni mwalimu wa
miaka mingi katika somo la Jiografia ambae anakiri kuwa, mwanafunzi
anapofundishwa darasani lazima apate kuona vitu katika uhalisia wake ili
kumjengea uelewa mapana zaidi juu ya anachokisoma.
Alisema ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri
katika somo la jiografia ni lazima awe na uelewa mpana kuhusu somo hilo, na awe
anajituma kutumia uelewa wake kujibu maswali mbalimbali yanayohusu somo hilo.
Mwalimu Mtegetwa amesema changamoto iliyopo
katika shule nyingi hapa nchini ni kwamba wanafunzi wanafundishwa viru ambavyo
hawajawahi kuviona kwa uhalisia wake hali inayopelekea kukosa kujiamini juu ya
kile wanachokisoma.
Akitolea mfano, Mwalimu Mtegetwa alisema
mwanafunzi anapofundishwa kuna mito inapita katikati ya milima anapaswa aone
hiyo milima na ni jinsi gani mto unaweza kupita katika hiyo milima.
Aidha, Mwalimu Mtegetwa alisema kuwa, kituo cha
Dar Nature ni kituo bora hapa nchini ambapo wanafunzi wanaweza kupata elimu ya
kutosha kwa kuona vitu kwa uhalisia wake.
Katika ziara iliyofanywa na wanafunzi wa kidato
cha tano na sita kutoka shule ya sekondari Aljebra kutembelea kituo cha Dar
Nature, wanafunzi wamekiri kufaidika na ziara hiyo ambapo wameweza kujionea
mambo mbalimbali yaliyowaongezea uelewa katika masomo yao.
Mwanafunzi wa kidato cha sita Tam Shabani Ntunda,
amesema amejifunza vitu vingi kupitia ziara hiyo ambayo imejaa elimu yenye
kujitosheleza kutokana na mazingira yaliyopo.
Nae Mwanafunzi Yasini Ngaguta wa kidato cha tano
amesema wameweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo uvumilivu katika
kukabiliana na changamoto ili kufikia malengo.
Alisema katika eneo la Dar Nature ndani yake kuna
njia zenye milima ambapo ili ufikie kwenye vituo vyenye masomo lazima upite
kwenye milima na hapo tulijifunza uvumilivu, kutokata tamaa na kujiwekea
malengo ya kufika pale unapokusudia.
Kwa upande wake Zainabu Ramadhani Alliy amesema
hakuwahi kufikiria kama ndani ya jiji la Dar es Salaam kuna eneo lina milima
ambayo mtu anashindwa kupanda, kwa ziara hiyo amesema ameshuhudia milima hiyo
ambayo darasani waliisoma na sasa ameona kwa uhalisia wake.
Swaumu Abbasi ni mwanafunzi wa kidato cha sita
amesema ni mara yake ya kwanza kufika Dar Nature lakini amefurahishwa na ziara
hiyo ambayo imemjengea uwezo kielimu kutokana na mambo mbalimbali aliyoweza
kuyaona katika eneo hilo na kujifunza.
Alisema miongoni mwa vitu walivyopata katika
kituo hicho ni SUPU YA ELIMU katika supu ya elimu waliweza kujifunza mambo
mbalimbali ikiwemo kutambua kuwa kusoma ni wajibu kwa kila mtu hivyo kila mmoja
anapaswa kuweka bidii katika kusoma ili kutimiza huo wajibu.
Mwalimu Hashim Idrisa Saleh ni Meneja wa shule za
Aljebra amepongeza uongozi wa Dar es Salaam Nature study na kusema kuwa ni
kituo bora kinachoweza kumjengea uwezo mwanafunzi katika masomo yake.
Aliongeza kuwa, ni wazi kuwa mwanafunzi anahitaji
kuona vitu kwa uhalisia wake ili kuongeza ari ya kujifunza na hatimae kufikia
malengo aliyojiwekea.
Alisema Dar Nature kuna utunzaji wa mazingira
mabapo ambapo mwanafunzi anajifunza utunzaji wa mazingira kwa kuona uhalisia
wake.
Kiongozi mwandamizi wa Dar es Salaam Nature Study, Mwalimu, Yasini Mkwizu amesema dhumuni kubwa la kituo cha Dar Nature ni
kutoa fursa kwa wanafunzi, walimu na wadau mbalimbali wa maswala ya elimu kuona
kwa uhalisia mambo mbalimbali ambayo wanasoma darasani.
Alisema kuna masomo mbalimbali ambayo wanafunzi
wanasoma darasani kama vile Sayansi, Jiografia, kilimo, lakini hawajakutana
navyo katika uhalisia wake.
Alisema walimu na wanafunzi ambao wameweza kufika
katika kituo cha Dar Nature wameweza kufaidika na mambo mbalimbali waliyoyakuta
katika katika kituo hicho.
Aliongeza kuwa, baadhi ya wanafunzi ambao
walikata tamaa ya masomo yao na kuyachukia wamerudisha matumaini yao mara tu
baada ya kutembelea katika kituo hicho.
Muongozaji wa kituo cha Dar Nature, Mwalimu
Selemani Kuliwa akitoa historia ya mto Nyebulu ambao umepita ndani ya eneo hilo, mbele yake ni wanafunzi pamoja na walimu kutoka Shule ya Sekondari Aljebra wakifuatilia kwa umakini maelezo hayo.
Kiongozi Mwandamizi wa Dar es Salaam Nature Study, Mwalimu, Yasini Mkwizu, akifafanua jambo kuhusu utunzaji wa mazingira wanafunzi wa Shule ya Sekondari Aljebra ambao walifika katika kituo hicho kwa ziara ya kimasomo.
Muongozaji wa kituo cha Dar Nature, Mwalimu
Selemani Kuliwa akiwaonyesha wanafunzi wa Sekondari ya Aljebra, milima iliyopo katika eneo hilo.
Walimu
pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Aljebra wakifuatilia kwa umakini
maelezo yanayotolewa na muongozaji wa kituo cha Dar Nature Mwalimu
Selemani Kuliwa (hayupo pichani) walipofika katika kituo cha mapumziko cha MPOPOMA kilichopo ndani ya eneo hilo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Aljebri wakipanda moja ya mlima uliopo katika eneo hilo ili kuelekea kituo kinachofuata cha mapumziko na masomo ndani ya eneo hilo la Dar Nature.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Aljebra, wakipumzika baada ya kumaliza kupanda mlima Togwa uliopo katika eneo hilo la Dar Narure.
Meneja wa shule za
Aljebra, Mwalimu Hashim Idrisa Saleh, akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG.
Mwalimu mzoefu wa somo la Jiografia Mng'ala Abdallaah Mtegetwa.
Ndani
ya eneo la Dar Nature utakutana na vibao vinavyotoa maelekezo ya vituo kwa
majina kama inavyoonekana katika kibao hicho
No comments:
Post a Comment