Afisa Michezo wa Wilaya ya
Bagamoyo, Vedastus Mziba akishiriki (kushoto) mazoezi ya kukimbia pamoja na vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, kwa pamoja walifanya mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17, macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.
................................................
Wito umetolewa kufanya mazoezi ya mara kwa mara
ili kulinda afya ya mwili kutokana na magonjwa mbalimbali.
Akizungumza mara baada kumaliza mazoezi
yaliyoandaliwa na Bagamoyo Joging mjini Bagamoyo, Afisa Michezo wa Wilaya ya
Bagamoyo, Vedastus Mziba amesema mazoezi huweka mwili katika hali ya usalama wa
kiafya na kuepukana na magonjwa mbali mbali.
Aidha, alisema kuwa michezo ni ajira na ni sehemu
ya kufikisha ujumbe kwa vitendo kwakuwa wana michezo wanapaswa kuwa mfano wa
kuigwa katika mambo mabli mbali ili jamii ijifunze kutoka kwao.
Aidha, aliwapongeza viongozi wa Bagamoyo Joging
kwa kuandaa mazoezi hayo ya kukimbia ambapo wameweza kushirikisha kikundi cha
mazoezi ya kukimbia cha Harakati kutoka Temeke jijini Dar es Salaam.
Alisema ilikufanikisha mazoezi vizuri
kunahitajika mipango itakayosaidia kupanga ratiba na kufikia malengo ya
yaliyokusudiwa kwa kikundi.
Awali akizungumza mara baada ya kuhitimisha
mazoezi hayo, Mwenyekiti wa Bagamoyo Joging, Hanga J. Mgumila amesema wameandaa
mazoezi hayo ya kukimbia na kuwaalika kikundi rafiki cha harakati kutoka Temeke
jijini Dar es Salaam, ili kuwaunganisha vijana katika mtazamo mmoja
utakaowafanya waweze kushirikiana katika mambo mbalimbali.
Alisema kikundi cha Bagamoyo Joging kimepata
mafanikio katika kuwanganisha vijana kwenye mazoezi ya kukimbia jambo
linaloleta faraja kuona sio tu kukimbia bali vijana hao wanaweza kufanya mambo
makubwa zaidi kwa pamoja.
Akizungumzia kupiga hatua kwa kikundi cha
Bagamoyo Joging, Hanga alisema kikundi kimepiga hatua kwa kufanikiwa kusajili
katiba iliyopitishwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) hali inayowapa uwezo
wa kutimiza malengo yao kwa mujibu wa katiba yao.
Aidha, alimpongeza Afisa michezo, wilaya ya
Bagamoyo, Vedastus Mziba kwa kushirikiana na Bagamoyo Joging katika kila hatua
na hatimae kufanikisha kusajili katika ya kikundi hicho cha michezo.
Kwa upande wake katibu wa kikundi HARAKATI Joging
kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, Mboke Salim Mboke alisema vijana wakitumia
vizuri fursa ya michezo wanaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya michezo.
Alisema michezo ni sehemu ya kuwakutanisha watu
wenye fikra mbalimbali ambao umoja wao untakiwa uendelee hata nje ya michezo.
Mboke aliendelea kusema kuwa, kikundi cha
Harakati licha ya kufanya mazoezi ya kukimbia pia kinajihusisha na shughuli
mbalimbali za ujasiliamali ambazo zinawawezesha kuendesha maisha yao ya kila
siku.
Alisema vijana wenye fani mbalimbali ndani ya
kikundi ndio chachu ya kutoa elimu kwa wengine na hatimae kikundi kinajitegemea
kikiwa na bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na wana kikundi.
Mboke alimalizia kwa kuwashukuru Bagamoyo Joging
kwa suhirikiano walio nao hali iliyowapa moyo wa kuongeza juhudi za ushirikiano
baina ya vikundi hivyo ili kufanikisha malengo yao.
Vikundi vya Bagamoyo
Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam,
kwa pamoja wakiwa kwenye mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi
2019, katika mji wa Bagamoyo.
Vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, kwa pamoja wakiwa kwenye mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.
Vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, kwa pamoja wakiwa mazoezi ya viungo mara baada ya kukamilisha mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Bagamoyo Joging, Hanga J. Mgumila, akieleza machache mara baada kumaliza mazoezi ya kukimbia mapema leo asubui tarehe 17 machi 2019 katika mji wa Bagamoyo.
Kushoto ni Mwenyekiti
wa Bagamoyo Joging, Hanga J. Mgumila, katibu wa kikundi HARAKATI Joging
kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, Mboke Salim Mboke wakimsikiliza Afisa Michezo wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba (hayupo pichani) mara baada
kumaliza mazoezi ya kukimbia mapema leo asubui tarehe 17 machi 2019 katika mji wa Bagamoyo.
Picha ya pamoja, Afisa utamaduni wilaya ya Bagamoyo Vedastus Mziba (katikati) akiwa na Vikundi vya Bagamoyo Joging ya Bagamoyo na HARAKATI joging ya Temeke jijini Dare es Salaam, mara baada ya kumaliza mazoezi ya kukimbi mapema leo asubui tarehe 17 macchi 2019, katika mji wa Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment