Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa
akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa uendelezaji wa zao la Pamba
(Cotton Victoria) uliofanyika katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani
Mwanza.
........................................
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano
ya kuinua kilimo cha Pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini.
Makubaliano hayo yamejili wakati ambapo Brazil ipo katika hatua
kubwa za kimageuzi ya kilimo huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo
ambapo unatekelezwa katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania.
Mradi wa kuinua kilimo cha Pamba unaotekelezwa na Brazil nchini
Tanzania utajikita Zaidi hasa katika kuhakikisha wakulima nchini wanapata Pamba
mbegu bora na uzinduzi wa utafiti utamfikia mkulima ili aweze kuongeza tija.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ameyasema hayo jana
tarehe 11 Machi 2019 mara baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa
kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.
Mhe Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania
inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja kuimarisha
sekta ya kilimo huku katika zao la Pamba imejipanga kuhakikisha inazalisha
mbegu vipara za Pamba zitakazotosheleza kwa wakulima wote nchini na kuondokana
na utumiaji wa pamba manyoya ambayo
imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.
Alisema Wizara ya kilimo itakuwa na
jukumu la kushawishi wawezaji ili kuwekeza kwenye viwanda vya Pamba
nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na
kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
yam waka 2015-2020.
Aidha, alisema kuwa Serikali pia imejipanga kupanua
maabara za utafiti wa zao la Pamba ili kuimarisha ufanisi na tija ya zao hilo kwani
mafanikio ya kilimo yanategemea zaidi katika utafiti.
Mhe
Bashungwa ameishukuru serikali ya Brazil kwa utekelezaji wa mradi huo nchini
Tanzania ambao unatokana na mahusiano mazuri katika nchi hizo mbili inayoakisi
katika kufungamanisha kilimo
na uchumi wa viwanda.
Kadhalika
alisema serikali tayari imeanzisha vituo viwili vya kuzalisha Pamba mbegu
vipara katika mkoa wa Simiyu pamoja na Mkoa wa Tabora
Sehemu ya washiriki wa mradi wa
uendelezaji wa zao la Pamba (Cotton Victoria) uliofanyika katika kituo cha
Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa
Kilimo Mhe Innocent Bashungwa wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Balozi wa Brazil nchini Tanzania Bw H.E Antonio akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uendelezaji wa zao la Pamba (Cotton
Victoria) uliofanyika katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza,
Kulia kwake ni naibu Waziri wa kilimo mhe Innocent bashungwa.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Innocent Bashungwa akikagua shamba la mfano wa kilimo cha Pamba katika kituo
cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza, Jana machi 11, 2019.
No comments:
Post a Comment