Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya ya Bandari Tanzania (TPA) Deodedth Kakoko kushoto akikabidhi
madawati 76 kwa mkuu wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga kulia
........................................
NA
HADIJA HASSAN, LINDI
MAMLAKA
ya Bandari Tanzania (TPA) Kanda ya Mtwara imechangia Madawati 76
yenye thamani ya sh. Milioni 13 katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Mkoani humo ikiwa ni namna ya kurejesha faida waliyoipata
inayotokana na shehena za mizigo na meli
Makabidhiano
ya madawati hayo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Rahaleo
iliyopo katika Halmashauri hiyo yaliyoudhuliwa na Wazazi, Wanafunzi Viongozi wa
Serikali ya Wilaya pamoja na wadau mbali mbali wa Elimu wa halmashauri
hiyo
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA) Deodedth Kakoko alisema kuwa Mamlaka hiyo kila mwaka
imejiwekea utaratibu wa kutenga fedha ya kuchangia katika maeneo
waliyoyapa kipaumbele hasa ya elimu , Afya na Maafa yanapotokea
lengo likiwa kurudisha faida na kutambulisha Kiasi kilichopatikana
kwa wadau wanaoshirikiana nao
Alisema
kuwa kwa kutambua jitihada zinazofanya na Rais Magufuli ya
kutoa elimu bure kwa wanafunzi wameamua kumuunga Mkono kwa kuchangia madawati
hayo kwa kuwa elimu ndio msingi wa kila Mtoto hasa katika karne hii ya
sasa
“
Ndugu zangu katika maeneo yanayoweza kuleta maendeleo ya Binaadamu
lakwanza ni Elimu hii ni kwa sababu ukishakuwa na Elimu mengine yote yanafuata,
ukiwa na elimu utajua namna ya kufanya matibabu, ukishakuwa na elimu utatafuta
ufumbuzi kwa ajili ya Barabara, kwa ajili ya Maji sasa ni wajibu wetu
kama wadau kushirikiana kwa pamoja ili kuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi
ili kuweza kusoma vizuri”. Alisema Kakoko
Nae
kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Batista kihanza alisema
kuwa madawati hayo yatagawiwa katika shule tatu za Halmashauri hiyo
ambapo Shule ya msingi Rahaleo itapatiwa madawati 25 , Shule ya msingi
Muungano itapatiwa Madawati 25 na Shule ya Mnazi Mmoja itapata Madawati 26
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga aliushukuru uwongozi wa
Mamlaka ya Bandari (TPA) kwa mchango huo wa Madawati na kusema kuwa
mchango huo umefika katika wakati muafaka ambapo kama Wilaya ilikuwa na uhitaji
makubwa ya madawati
“
Tunaupungufu wa Madawati katika baadhi ya Shule na upungufu huu umetokana na
Sera ya Elimu bure, tunaandikisha Wanafunzi wapya na wanaongezeka mwaka
hadi mwaka lakini kama hiyo haitoshi tunao mkakati kama Wilaya wa
kuhakikisha tunakomesha utoro na katika juhudi hizi za kupambana na utoro ndio
tunajikuta sasa kuwa kumbe tunaingia sasa katika mpango mwingine wa
kuwarudisha watoto ambao waliacha Shule, kitendo hiki kinaongeza mahitaji ya
Viti na Meza , kinaongeza mahitaji ya Madawati kwa hivyo kama vile mlijua
kama tunao uhitaji katika eneo hili” alieleza Ndemanga
Ndemanga
pia alitumia fulsa hiyo kuwahasa wadau wengine kujitoa katika kuchangia
shuguli za kimaendeleo kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza kero
zinazowakabiri wananchi wa maeneo husika na hata kutawasaidia katika
kujitangaza kwa wananchi kutambua shughuli wanazozifanya
No comments:
Post a Comment