NA MWAMVUA MWINYI, MLANDIZI
MSAFARA wa Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo umezuiliwa na
watumiaji wa Stendi ,wafanyabishara wa soko na wauza mitumba
(WARUMBA) eneo la Mtongani Mlandizi ,wilayani Kibaha kupinga
kuhamia kwenye eneo jipya la Mama Salmini ambako wanadai hakuna maslahi
kwao.
Kufuatia hali hiyo ametoa maelekezo kuwa kutokana na soko
hilo kutokuwa mali ya serikali ni ya mtu binafsi kwa maslahi mapana ya wananchi
soko la mama salmini wawe huru na wale wanaotegemea Mlandizi waendelee huku
wakisubiri ukamilishaji wa soko jipya.
Kuhusu stendi ,Jafo amesema medereva daladala wanapata shida
na stendi wawe na uhuru chini ya usimamizi wa wilaya waendelee kutumia stendi
ya mlandizi hadi hapo stendi itakapokmilika.
Akizingumza na wafanyabiashara hao, alieleza wafanyabiashara
hao waachiwe wafenye biashara kwa utaratibu na kufuata sheria bila
kubughudhiwa.
“Nimeangalia idadi ya watu na eneo hilo la mama Salmini
wenye hiari ya kufanya biashara wafanye biashara kwenye eneo hilo,lakini na
wanaotegemea biashara Mlandizi waendelee “alisisitiza Jafo.
“Mnajengewa soko la kisasa na serikali ipo kwenye mchakato
wa kujengwa stendi mpya,hivyo taratibu nyingine zitafuata. “
Hata hivyo, Jafo alifafanua, Watu wadogo wasinyanyasike
ofisi ya mkuu wa wilaya na halmashauri iangalie utaratibu wa kuwasogeza kwenye
eneo lisilo hatarishi na wafanya biashara wafuate utaratibu, sheria na
utaratibu hadi hapo soko maalum litakapokamilika.
“Wafanyabiashara toeni ushirikiano na serikali ya chama cha
mapinduzi kwa maslahi ya wilaya na mkoa. “alisema Jafo.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,aliwataka
wawe watulivu na kutoa ushirikiano kwa serikali.
Jumaa alisema agizo la Jafo lipo sawa kwa maslahi ya
wafanyabiashara hao wanyonge.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Warumba ,Nasoro Soma alisema
kuwa wao hawako tayari kwenda kufanyabiashara kwenye soko jipya kutokana na
mazingira yake hayako vizuri kibiashara .
Alisema Rais Dk John Magufuli hakukosea kumteua Jafo kwakuwa
yupo makini kutekeleza kazi zake na kufuatilia mambo.
No comments:
Post a Comment