GURUMO AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI KIKWETE
Na Omary Mngindo, Kimange
DIWANI wa Kata ya Kimange Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Pwani Juma Gurumo, amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu na Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kuiangalia kwa jicho la kipekee.
Gurumo ametoa kauli hiyo Sept 17 akipokea mabomba yanayolenga kuboresha upatikanaji wa Maji, kutoka kutoka kwa Ofisa wa DAWASA Mhandis Kahemele, ambapo alisema Serikali imeonesha namna gani inavyowajali wanaKimange.
"Nielezee shukrani zangu kwa Serikali yangu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu pamoja na Waziri wa Utumishi Ridhiwani Kikwete ambae ndio Mbunge wangu, Kimange inakwenda kwa kasi kubwa," alisema Gurumo.
Aliongeza kuwa ameingia kwenye nafasi hiyo akiwa mwenye bahati kubwa, kwani tangu achaguliwe mwaka mmoja uliopita kumekuwepo na kasi kubwa ya maendeleo yanayoelekezwa katani kwake.
"Nimeingia na bahati kwani kwa kipindi kifupi tangu nichaguliwe kuwa Diwani Maji yanazidi kuongezewa miundombinu, sasa yanapatikana maeneo mengi na leo tunapokea mabomba zaidi lengo kuongeza upatikanaji wa huduma," alisema Gurumo.
Aliongeza kuwa "Mbali ya zoezi ili muhimu, Jumanne tunataraji kumpokea Mkandarasi wa kuchonga Barabara, naishukuru Serikali yangu pamoja na Mkurugenzi Ramadhani Possi, Madiwani wenzangu na Wataalamu wote," alisema Diwani huyo.
"Kwa umoja wetu wanaKimange tunawashukuru Rais Dkt Samia na Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kutupambania, sote ni mashuhidi tunaona utatuzi wa changamoto hakika tunaelekea kwenye Kimange mpya," alisema Gurumo.
Alimalizia kwa kusema kuwa mabomba hayo ya awamu ya kwanza yanakwenda kubadilisha yaliyokuwa chakavu kwa umbali wa kilometa 4 kutoka Kijiji cha Kimange kwenda Pongwe Kiona na Pongwe Mnazi.
Kwa upande wake Mhandis Kahemele alisema kuwa Taasisi hiyo chini ya Meneja wake Boniface Ole wanaendelea na kazi ya kuhakikisha adha ya Maji Jimboni humo inabaki historia.
"Tunaishukuru Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu, Waziri wetu Jumaa Aweso na Waziri Ridhiwani Kikwete (Mbunge) ambao wanatuwezesha katika kutatua changamoto ya Maji kwa wanaChalinze," alisema Mhandis Kahemele.



Comments
Post a Comment