TAKUKURU KAGERA YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 2.

 

Na Alodia Babara, 


Bukoba.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imefanikisha uokoaji wa zaidi ya sh bilioni 2.7 kutoka kwa makampuni binafsi 146 yaliyokuwa wadaiwa sugu wa michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kati ya jumla ya Sh5.2 bilioni zilizokuwa zinadaiwa.


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kagera Ismail Bukuku akizungumza na waandiahi wa habari Septemba 16, 2026

amesema, hatua hiyo imechukuliwa baada ya ofisi yake kufuatilia madeni hayo na kuchukua hatua dhidi ya waajiri waliokuwa hawawasilishi kwa wakati fedha za michango ya wafanyakazi wao katika mfuko huo.


"Waajiri hawa walishindwa kulipa michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia mwaka 2017 hadi Julai 2026 iliyofikia kiasi cha sh bilioni 5.2" amesema Bukuku


Alieleza kuwa, oparasheni hiyo ilifanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza oparasheni ilianza Julai 22 hadi Agosti 5 huku awamu ya pili ilifanyika Agosti 17 hadi Agosti 31,2026


Ameeleza kuwa, baada ya kuanza kwa  ufuatiliaji wa fedha za michango husika katika awamu ya kwanza TAKUKURU ilifanikiwa kuokoa kiasi cha sh bilioni1.6 sawa na asilimia 31 ya michango inayodaiwa.


Aidha, katika awamu ya pili ya oparasheni timu ya ufuatiliaji ilifanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya sh bilioni 1 na kufanya jumla ya fedha yote iliyookolewa kufikia sh bilioni  2.7 sawa na asilimia 52 ya michango inayodaiwa.



Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zaidi ya nusu ya fedha zilizokuwa zinadaiwa tayari zimekusanywa, huku jitihada zikiendelea kuhakikisha kiasi kilichosalia kinakusanywa kwa asilimia 100 na kuwasilishwa NSSF kwa ajili ya kulinda haki na mafao ya wafanyakazi.




Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.