Naibu Waziri wa Nishati Mhe.
Bi. Subira Mgalu, Akizungumza wanafunzi wa Shule ya Msingi Chalinze Mzee
iliyopo Chalinze Mkoani Pwani kabla ya kuzindua na kuwasha Umeme rasmi katika
kijiji cha Chalinze Mzee Mkoani Pwani.
..................
Na
Yasini Silayo, Pwani
Naibu
Waziri wa Wizara ya Nishati Mhe. Bi. Subira Mgalu akizindua na kuwasha rasmi
miradi ya Umeme Vijijini katika Vijiji vya Chalinze Mzee A-C na Nero Vilivyoko
Chalinze, Mkoani Pwani Leo ametoa Rai kwa vijiji vyote ambavyo tayari
vimefikiwa ama kuunganishwa na huduma ya Nishati ya Umeme kuitumia fursa hiyo
kuboresha ufaulu pamoja na kuinua kiwango cha elimu kwa ujumla.
“Ni mategemeo yetu kuwa ujio na matumizi ya Nishati ya umeme utaboresha na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kutokana mazingira wezeshi ya kujisomea na kujifunza muda wote kwa kutumia mwanga wa umeme lakini pia kuendana na mahitaji ya elimu ya kisasa inayojikita zaidi katika sayansi na teknolojia hususan matumizi ya kompyupa na maabara za kisasa za mafunzo kwa vitendo” Alisema Mhe. Subira, Akiwa katika shule ya Msingi Chalinze Mzee kijiji Cha Chalinze mzee A, Mkoani Pwani.
Naibu Waziri Mgalu, Aliongeza kuwa, Ndoto ya Serikali ya Awamu ya Tano ni, kusambaza Nishati ya umeme Nchi Nzima na kwa wananchi wote, umeme utakaokuwa chachu ya maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo za Maendeleo ya Huduma za kijamii sambamba na zile za Kiuchumi, sekta ya elimu kwa vijana na watanzania kwa ujumla ikiwemo kama miongoni mwa sekta za vipaumbele.
Naye mwalimu mkuu wa shule hyo aliyejitambulisha kwa jina la Marianus Nyalale, mbali na kuelezea shukurani zake kwa kufikishiwa umeme mpaka shuleni hapo, alisema kuwa Shule ina matarajio makubwa ya kufanya mabadiliko makubwa ya kiufundishaji na ufaulu mara baada ya kuunganishwa na huduma ya umeme wa TANESCO.
“Tunategemea kuanza mpango wa kutafuta fedha kwaajili ya kununua compyuta na vifaa mbali mbali vya kufundishia vinavyotumia umeme lakini pia hivi sasa wanafunzi wataweza kujisomea madarasani hata vipindi vya jioni” alisema Mwl. Nyalale
Aidha, Mhe. Mgali akizindua na kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Nero, alisisitiza na wananchi pia kuchangamkia fursa ya umeme kwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaemdeleo na kiuchumi.
Shughuli zitakazopelekea wao kujiongezea kipato lakini pia kukuza uchumi wa Nchi kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment