Waziri wa
Elimu,Sayansi na Teknolojiaa Profesa Joyce Ndalichako anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika mkutano wa kimataifa wa waratibu wa kitaifa wa miradi
inayotekelezwa na Shirika la nguvu za Atomiki duniani kwa nchi 46 kanda ya
Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 mwezi Machi 2019 jijini Arusha wenye
lengo la kujadiliana na masuala mbali mbali.
Mkutano huo utashirikisha washiriki 60 kutoka nchini 46 duniani kutoka baara la AFRIKA ambao ni wanachama wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani kwa pamoja wataweza kujadiliana masuala mbalimbali.
Mkurugenzi
mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ,Profesa Lazaro Busagala amaesema
maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwamba wana imani mkutano huo utaweza
kusaidia nchi washiriki kuweza kusonga mbele katika namna ya uboreshaji wa
sekta mbali mbali kutokana na miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la
Nguvu za Atomiki Duniani(IAEA).
Pia Profesa Busagala ameongeza kuwa mkutano huo pia utahudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki kanda ya AFrika Bwana Shaukat Abdurazak ambaye baada ya mkutano huo ataweza kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali na uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Wizara nne ambazo zimekuwa zikihusika katika miradi mbali mbali ya kitaifa inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duninia(IAEA) .
Alisemsa
kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mkurugenzi Shaukat atakutana na
Waziri wa
Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi .
Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi .
Kwa upande
wa Tanzania Bara Shaukat atafanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, na Waziri wa Maji.
Pia ataweza
kufanya ziara katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Seliani,Taasisi ya Chakula na
Lishe na Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Profesa Busagala alisema kuwa
mazungumzo hayo yataweza kusaidia nchi kwenye uboreshaji wa miradi mbali mbali
inayofanyika hapa nchini hasa katika sekta ya Afya, Kilimo, na maji.
Alieleza
kuwa Tanzania ni moja ya nchi iiliyoweza kufaidika kwa kiasi kikubwa kwa miradi
katika udhibiti na kuhamasisha matumizi salama ya tekenolojia ya nyuklia
inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duniani .
No comments:
Post a Comment