Mabadiliko
hayo ya alama ya utambulisho wa kampuni yamelenga kuenda sawia na malengo ya
kampuni katika huduma za usafirishaji ambapo mpaka sasa tayari imepanua huduma
za safari zake kwenye magari na pikipiki.
Akizungumza
na na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu mabadiliko hayo
Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi mwenza wa Bolt, Markus Villig, alisema jina
hilo jipya la Bolt litaanza kufahamika hatua kwa hatua katika masoko ya
kimataifa katika wiki zijazo.
Alisema
Taxify ilizinduliwa miaka mitano iliyopita kwa malengo ya kutoa huduma za
usafiri mijini kwa njia rahisi na bei nafuu.
“Kampuni
hiyo ya kiteknolojia kutoka Estonia imefanikiwa kukua na kuvuka mipaka tangu
kuanzishwa kwake ambapo sasa imewafikia wateja milioni 25 katika nchi zaidi ya
30 duniani, na kuifanya kuwa kampuni inayoongoza barani Ulaya na Afrika.
“Ilikuwa
pia kampuni ya kwanza ya kurahisisha huduma za usafiri na kwa sasa inafanya
kazi katika kupanua huduma ya usafiri wa pikpiki kwenye miji kadhaa ya Ulaya,”
alisema.
Aidha,
Meneja Mkazi nchini Tanzania kutoka Bolt, Remmy Aseka alisema bidhaa ya
kwanza ya kampuni hiyo ya usafirishaji ilikuwa ni kutoa suluhisho la
kurahisisha upatikanaji wa huduma za teksi kwa wateja wake.
“Tumefanikiwa
kuongeza uboreshaji katika malengo yetu, tumeanza pia kukuza jina la kampuni
yetu katika maeneo mbalimbali. Lengo letu ni kutatua matatizo ya usafiri kwa
kiwango kikubwa zaidi, tunataka jina la kampuni liendane na mambo yajayo ya
kampuni na sio yaliyopita. Jina jipya la ‘Bolt’ linamaanisha kufanya jitihada
bila kutumia nguvu, hasa uzoefu wa kuzunguka katika mji kwa gari, pikipiki au
usafiri wa umma.
“Pia
inaendana na matarajio yetu kuwa baadaye huduma za usafirishaji zitakuwa kwa
njia ya umeme. Pia watumiaji wa Bolt hawatahitaji kufanya mabadiliko yoyote
kwenye program zao kwa kuwa Bolt itajibadilisha moja kwa moja kwenye program
hizo,” alisema.
No comments:
Post a Comment