Na
HADIJA HASSAN, LINDI.
BAADHI
ya kaya zinazoishi katika Manispaa ya Lindi Mkoani humo zinatumia vyoo ambavyo
havijaezekwa kwa madai kuwa wanashindwa kupumua vizuri wakati wa kujisaidia
Hayo
yameelezwa na Afisa afya wa Manispaa hiyo jana alipokuwa anazungumza na
Bagamoyo kwanza blog afisini kwake ilipotaka kufahamu juu ya namna ya kampeni
ya “USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO” inavyotekeleza na ilipofikia
Seiph
alisema kuwa licha ya Kampeni hiyo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini bado
baadhi ya Wananchi wa maeneo hayo hawana uelewa wa umuhimu wa kutumia Vyoo bora
Ni jambo la kushangaza kuona kuwa wakati tukiendelea na Kampeni hii
tukitembea mtaa kwa mtaa, kata kwa kata nyumba kwa nyumba tuliweza
kubaini kuwa zipo baadhi ya kaya zikitumia vyoo ambavyo havijaezekwa kwa madai
kwamba wanashindwa kupumua vizuri wakati wa kujisaidia
“
wakati tunaanza kampeni hii ya usafi wa Mazingira kwa ujumla Manispaa yetu ya
Lindi ilikuwa na asilimia 36 ya wakaazi kwa maana ya nyumba zenye vyoo Bora,
lakini mpaka sasahivi tumeweza kufanikisha zoezi hili kwa kuongeza idadi
ya kaya ambaozo zina vyoo bora kwa zaidi ya asilimia 55 sawa na kaya 8339
kati ya kaya 20006” alisema Seiph
Hata
hivyo Seiph alisema mpaka sasa Manispaa hiyo kaya ambazo zina vyoo
pasipo kuzingatia ubora ni kaya asilimia 99.3 ambapo kati ya hizo kaya zenye vyoo
bara ni asilimia 55.2 na kaya asilimia 44.4 zinavyoo ambavyo havina ubora huku
asilimia 0.2 zikiwa hazina vyoo kabisa
Aidha
Seiph aliongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo wapo baadhi ya
wananchi ambao bado wamekuwa wakijisaidi vichakani kwa wale wanaoishi pembezoni
mwa mji na wapo baadhi ya wananchi wanaojisaidia ufukweni kwa wale ambao
wanaishi pembezoni mwa bahari
Seiph
pia alitumia fulsa hiyo kuwahasa wananchi wa Manispaa ya Lindi kuacha tabia ya
kujisaidia vichakani sambamba na kwenye fukwe za bahari kwani kwa kufanya hivyo
kunaweza kuhatarisha afya zao hii ni kutokana na hata wale waliojenga vyoo bora
wanaweza kuwahatarini kupata ugonjwa wa matumbo
No comments:
Post a Comment